Umejipunja Vya Kutosha! Jikumbuke Ujenge Utajiri Wako..


Categories :

Kama ukiambiwa upige hesabu ya fedha zote ambazo umewahi kuzipata tangu uzaliwe, utashangazwa sana kwa nini wewe mpaka sasa siyo tajiri!

Kama fedha zako zote ulizozipata
[  ] Ulinunulia nguo, basi ulimpendelea mwenye nguo, wewe ukajisahau.
[  ] Ulinunulia chakula, basi ulimpendelea muuzaji, wewe ulajisahau.
[  ] Kama ulinunulia gari, basi ulimpendelea mfanyabiashara huyo, wewe ukajisahau.
[  ] Ulilipa ada, basi ulimpendelea mwenye shule, wewe ukajisahau

Kama kila fedha unayoipata unaitumia yote bila kubakiwa na kiasi chochote,  basi tambua umekuwa ukijipunja sana na huna budi kubadilika haraka sana.

Kuna kanuni ya dhababu ambayo matajiri wote wameitumia kujenga utajiri wao. Habari njema njema ni kuwa hata wewe unaweza kuiishi na kujenga utajiri maishani mwako.

Kanuni hii inaitwa “Jilipe Wewe Mwenyewe Kwanza”. Kwenye kila fedha unayopata, hatua ya kwanza kabisa unayotakiwa kuichukua ni kuhakikisha unatenga angalau 10% ya fedha yako kisha unaendelea na mipango mingine na fedha inayobaki.

Hii 10% ni mbegu ya utajiri wako..
Weka kila fedha hiyo sehemu inayoweza kuzalisha zaidi kwa mfano kwenye vipande, hisa, hatifungani, majengo nk.

Ukifanya hivyo kwa msimamo na muda mrefu utajenga utajiri na uhuru wa kifedha maishani mwako.

Inawezekana ulijipunja kwa kutokujua…kwa sababu sasa umeifahamu siri hii hakikisha hujionei tena. Usiische fedha yoyote ikapita mikononi mwako bila kujilipa.  Ukishindwa 10% basi anza na 5% au 2%. Anza hata na 1% kisha endelea kukua ukijenga nidhamu hii muhimu maishani mwako.

Kanuni hii ni mojawapo ya miongozo ya kufikia uhuru wako wa kifedha iliyopo kwenye kitabu cha SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA. Hakikisha umekipata kitabu hiki ili kuianza au kuongeza kasi ya kujenga uhuru wa kifedha maishani mwako.

Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala chache za ofa zilizobaki.

Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Trainer,  Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *