Nguzo 8 Muhimu Za Maisha Ya Mafanikio.
Nyumba imara hushikiliwa kwa nguzo imara tena za zege. Kadhalika maisha yako ya mafanikio yanashikiliwa na nguzo imara za mafanikio.
Kama hujaanza kuyaona mafanikio kwenye maisha yako, au maisha yako yanasuasua basi anza kujenga nguzo hizi 8 muhimu za mafanikio.
1. Mtazamo chanya.
Unachokiamini ndicho unachokipata. Utaanza kupata matokeo ya utofauti pale utakapoanza kujiona unaweza.
2. Kazi kubwa.
Mafanikio ya uhakika yanajengwa na kazi ..tena kazi kubwa. Acha kuendelea kusubiri bahati..weka kazi kubwa.
3. Nidhamu.
Baada ya kuweke malengo na mipango mizuri kinachofuata ni kujisukuma kuchukua hatua. Hata ukikutana na ugumu..wewe endelea.
4. Jiamini.
Kuna wakati hakuna hata mmoja atakayeamini kwenye ndoto kubwa uliyonayo. Huo utakuwa muda wa kuuonyesha upekee wako..wewe endelea.
5. Msimamo.
Ni mafanikio madogo ndiyo huzaa mafanikio makubwa…ukianza usiache. Mafanikio ni 5% akili na 95% msimamo.
6. Kafara.
Ili kufikia mafanikio makubwa unayoyata huna budi kuacha vingi vinavyokulia muda, nguvu na fokasi lakini visivyo na mchango kabisa au mdogo kwenye ndoto yako.
7. Fokasi.
Wakati ukifanyia kazi ndoto zako lazima utakutana na vikwazo pia. Vikwazo hivyo visikutoe kwenye reli, baki kwenye mipango yako. Usikimbilie kila fursa utakayokutana nayo.
8. Uvumilivu.
Angali ukiwa kwenye njia sahihi, ukikutana na magumu vumilia, matokeo yakichelewa wewe vumilia, wakikukatisha tamaa wewe vumilia.
Hakuna kitakachokukatisha kupata unachokitaka kama hutakata tamaa.
Kuendelea kuimarisha nguzo hizi muhimu za kujenga mafanikio ya kudumu ya maisha yako hakikisha unajipatia kitabu chako cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO.
Kwa kuwa na kitabu hiki utafanikiwa kutumia dakika 5 tu kusoma DONDOO moja kila siku kwa mwaka mzima bila kujirudia. Hii itakufanya kuwa na siku yenye mafanikio makubwa kwa mwaka mzima.
Habari njema ni kuwa leo utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa kabisa, tsh 3,000 tu. Tuma fedha yako mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Utapokea kitabu chako ndani ya dakika 3 tu. Of hii ni ya leo tu.
Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Trainer, Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.