Mbinu 6 Za Kuanzisha Biashara Baada Ya Kuahirisha Kwa Muda Mrefu.
Je kila wakati ukijipima unajiona bado hujawa tayari kuanzisha biashara?
Je unaona mtaji hautoshi? Je unaona huna eneo la kufanyia biashara? Je unaona huna wateja? Je unaona kama bado una muda?
Kama ndivyo umekuwa unajiona, basi tambua umeendelea kubembeleza uwezo wako wa kuanzisha na kukuza biashara kuendelea kulala. Hivyo umekosa fursa za kukuza kipato chako.
Zifahamu na tumia mbinu hizi 6 ili kutoka kwenye mkwamo uliokaa hapo kwa siku nyingi.
1. Anzia hata hapo chini.
Licha ya kuwa na ndoto ya kuwa na biashara kubwa …lakini unaweza kufika huko kwa kuanzia hata hapo chini. Anzia chini kisha nenda juu.
2. Anza na unachokifahamu.
Hakuna siku utasema sasa na fahamu kila kitu kuhusu biashara ya ndoto yako.
Anza na maarifa machache uliyonayo….kisha endelea kuongeza angali ukiendelea kuikuza biashara yako.
3. Anza na unavyomiliki.
Je umekuwa ukiajiambia huwezi kuanzisha biashara kwa sababu huna mtaji? Kuna vitu unavyovimiliki tayri, anza na hivyo.
[ ] Anza na nguvu zako
[ ] Anza na kipaji chako
[ ] Anza na vitu unavyovimiliki lakini huvitumii sana; jokofu, oveni,…
4. Anza na wanaokuzunguka.
Watu unaofahamiana nao; waliopo kwenye simu yako, majirani, wafanyakazi wenzako ni wateja wa kwanza wa biashara yako…anza nao.
5. Anzia Hata Nyumbani
Usiache eneo maalumu la kufanyia biashara kuwa kikwazo kwako. Anza hata kuuzia nyumbani. Nunua bidhaa zako(nguo, nafaka, urembo nk) weka nyumbani kisha anza kupiga, kuwatembelea wateja au kupost kwenye mitandao…ukipata mteja unampelekea bidhaa kutokea nyumbani.
6. Anza Leo.
Umeahirisha vya kutosha ukidhani kuna muda mwingine. Hakuna muda mwingine mzuri. Jisukume kuanza leo.
Kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA kimewasaidia wengi kuanzisha na kukuza biashara zao baada ya kusuasua kwa muda mrefu?
Ni zamu yako sasa kufanikiwa kuanzisha au kukuza biashara yako iliyolala siku nyingi. Jipatie nakala yako sasa ikuongoze njia sahihi ya kuongeza kipato chako ulichokikosa siku nyingi. Wasiliana nasi kujipatia nakala yako leo.
Anza Leo Anza Sasa Anza Na Chochote Ulichonacho.
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Trainer, Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.