Fedha Zilizochakaza Pochi Yako Umezipeleka Wapi?


Categories :

Kama pochi yako imechakaa ni ishara kuwa kuna fedha nyingi zimekuwa zikiingia humo.

Swali muhimu la kujiuliza ni wapi umezipeleka fedha hizo?

Kama kuna fedha nyingi ziliingia kwenye pochi yako na kuichakaza lakini hakuna fedha yoyote uliyobakia nayo, basi huu ni ushahidi tosha kuwa kila fedha iliyopita mikononi mwako,  uliitumia yote.

Kama kila fedha itakayopita mikononi mwako utaitumia yote, basi tambua kuwa itakulazimu kuitafuta fedha maisha yako yote …hata pale utakapokuwa mzee na nguvu zimekuishia.

Habari njema ni kuwa unaweza kuepuka utumwa huu kwa kuhakikisha unajilipa mwenyewe kwenye kila fedha unayoipata.

Kwenye kila fedha unayoipata hakikisha unatenga angalau 10% na kuiwekekeza ili iendelee kuzaa fedha nyingine kubwa zaidi.

Hii itakuwa ni mbegu ambayo itaendelea kukua na kukuzalishia fedha nyingi bila ya wewe kufanya kazi moja kwa moja.

Kitabu chako cha SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA ni mwongozo wa kukuondoa kwenye utumwa wa kudumu wa kifedha kisha kukusaidia kujenga uhuru wa kifedha.

Jipatie kitabu hiki leo ili uianze au uongeze kasi ya kujenga uhuru wako wa kifedha.

Hata hivyo ukikipata kitabu hili leo, utapata ofa ya kuingia kwenye Programu ya STAAFU UKIWA HURU KIFEDHA ambako utaungana na watu wengine kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji kwenye VIPANDE, HISA & HATIFUNGANI. Pia utajenga nidhamu ya kuwekeza kila mwezi bila ya kuacha mpaka ufikie uhuru wa kifedha.

Rafiki kama kweli unataka kuwa huru maishani mwako, hili ni jambo unalotakiwa kilipa uzito mkubwa leo.

Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kukipata kitabu hiki kisha kuanza kujenga nidhamu ya kuwekeza kwa msimamo mpaka ufikie uhuru wako wa kifedha.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer

AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *