95% Ya Mafanikio Yako Yamejificha Hapa…..
Kama kuna siri kubwa umekuwa ukiitafuta juu ya kupata mafanikio, basi leo utaifahamu.
95% ya mafanikio ambayo umeyatafuta kwa siku nyingi ipo yamejificha kwenye msimamo. Ndiyo MSIMAMO.
Msimamo ni kufanya kitu kimoja kwa kujirudia rudia bila kuacha mpaka upate matokeo unayoyataka.
Licha ya kuweka nguvu ili kupata mafanikio lakini hujafanikiwa kwa sababu umekuwa mtu wa kugusa na kuacha.
[ ] Ulianzisha biashara, ulipoona hupati faida ukaifunga hata kabla ya wateja wengi kujua unachouza.
[ ] Kila wakati umekuwa ukiacha kile ambacho unakifanya kisha kukimbilia kwenye fursa mpya.
[ ] Umekosa ustahimilivu, kila changamoto imekuwa ikikutoa kwenye reli.
[ ] Umekuwa ukiwekeza kwa muda mfupi kisha kuacha kwa sababu ya kutaka matunda ya uwekezaji ndani ya muda mfupi tu.
[ ] Umekuwa ukianza kujenga tabia mpya za mafanikio lakini kabla haijakamilika umekuwa unarudi nyuma. Mbona ulianza kuamka mapema lakini sasa umerudia utaratibu wa zamani wa kuchelewa kuamka?
Matone ya mvua hujaza pipa kwa kuendelea kudondoka kwa msimamo kwenye pipa hilo.
Lakini pia matone ya mvua yakiendelea kudondoka kwenye zege, hufanikiwa kuchimba shimo kwenye zege hilo ngumu.
Msimamo ndiyo utakaolainisha yale yanayoonekana magumu sasa.
Chukua Hatua:
Chagua kitu kimoja chenye fursa ya kukua hata kama utaanza kidogo kisha jitoe kukifanya hicho kwa msimamo bila kuacha.
[ ] Je biashara gani hiyo?
[ ] Je ni kujilipa wewe kwanza 10% ya kila kipato chako
[ ] Je ni kusoma vitabu kila siku?
[ ] Je ni kuwekeza kwa msimamo?
[ ] Je ni kuamka mapema kila siku na kuwa na siku yenye mafanikio?
Msimamo ni miongoni mwa hatua 10 za kuchukua ili kuweka na kutimiza malengo yako zilizopo kwenye kitabu cha MWONGOZO WA KUTIMIZA MALENGO YAKO. Jipatie kitabu hiki leo kikusaidie kupata mafanikio uliyoyakosa siku nyingi.
Habari njema ni kuwa utakipata kitabu hili leo kwa bei ya ofa sh 3,000 tu. Tuma fedha yako mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Utapokea kitabu chako ndani ya dak. 3.
Karibu sana.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899