Ndoto Kubwa Huanza Hata Kwa Udogo….
Ndoto yako kubwa haifikiwi kwa siku moja….bali kwa siku nyingi zilizoambatana na msimamo wa hatua sahihi.
[ ] Kuwa na ndoto kubwa kwenye kile unachokitaka kubobea…lakini ongeza maarifa na ujuzi kwenye eneo hilo kila siku.
[ ] Hata kama ndoto yako ni ya miaka 10 lakini jikumbushe ndoto hiyo kila siku.
[ ] Hata kama biashara yako ina wateja wachache sasa….kumbuka hao ndiyo wa kuleta wateja wa kuikuza biashara yako.
[ ] Hata kama leo hutayaona matokeo…endelea kukifanya kilichosahihi kwani muda wa mavuno utafika…hakuna thamani ambayo huwa inapotea bure.
[ ] Akiba ndogo inayowekezwa kwa msimamo ndiyo itakayokupa utajiri miaka 10 ijayo….usiache kuwekeza.
[ ] Mahusiano mazuri unayoyajenga ni mtaji wa mafanikio yako mbeleni.
Nyumba ya ndoto yako kujengwa kwa tofari za vitendo sahihi utakavyovifanya kila siku.
Usiache kufanya kitu kila siku hata kama ni kidogo kwa ajili ya ndoto yako.
Karibu sana.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899