Siri Ya Kuacha Kujidharau Kisha Kuanza Kufanya Makubwa…..
Kuna watu zaidi ya bilioni nane duniani lakini kuna WEWE mmoja tu.
Kuna mtu kafanana sasa na wewe kwa nje lakini WEWE wa ndani yako hafanani na yoyote.
Unaweza kukimbia vitu vyote lakini sio kivuli chako.
Wanaweza kuona vyote vilivyo nje yako lakini siyo kile unachokiumba ndani yako.
Watu wanaweza kutengeneza vitu vingi lakini ukitengeneza chako kitakuwa cha pekee.
Kuna WEWE mmjoa tu dunia hii na hatatokea mwingine kama WEWE.
Thamani yako ni kubwa hakuna cha kufananisha.
UKUU wako, UTAJIRI wako, UMAARUFU wako, UTOSHELEVU wako…..upo kwenye upekee wako.
Kuna kitu unaweza kukiumba na kukifanya kwa viwango vya juu sana ukiwa WEWE HALISI.
Ili kuuona upekee wako, sikiliza moyo wako badala ya kujidharau kwa maoni ya wengine.
Jiulize swali hili na kujisikiliza mpaka upate jibu; una upekee gani ndani yako?
Habari njema ni kuwa kila mtu ana upekee ndani yake, ikiwa ni pamoja na wewe.
Jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kuanza nalo mwaka mpya 2025 ni kutambua na kuanza kuuishi upekee wako.
Huu ndiyo msingi wa kufikia ndoto yako kubwa ambayo umekuwa na wasiwasi kama utaitimiza.
Sasa usiwe na wasiwasi, kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kitakuongoza kutambua uwezo wako wa kipekee utakaokusaidia kupata mafanikio makubwa unayostahili hapa duniani.
Bonyeza kiunganishi hapa chini kujipatia kitabu chako sasa https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/66/
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899