![](https://www.amshauwezo.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250206-054757_Chrome.jpg)
Je Unataka Kujenga Utajiri? Basi Jifunze Kwa Huyu Mkulima Makini.
Wakati nikiwa bado mdogo kuna kitu ambacho nilikuwa nakiona wakifanya wazazi ambacho sasa natambua kuwa kumbe walikuwa wakiishi kanuni hii muhimu ya fedha.
Baada ya kuvuna tu mahindi, kabla hawajayapukuchua, walikuwa wanachagua mahindi ambayo yamekomaa vizuri, yenye punje kubwa na ambayo hayajaathiriwa na wadudu kisha kuweka pembeni. Baada ya kufanya hivyo ndipo walipukuchua mengine kwa ajili ya matumizi ya chakula au kuuza.
Yale mahindi machache na mazuri waliyokuwa wameweka pembeni, waliyatunza sehemu nzuri ambapo hayawezi kuharibika. Hayo yalitumika kama mbegu kwa ajili ya msimu ujao wa kupanda.
Lakini kilichokuwa kinanishangaza zaidi, hata pale tulipokuwa tuna uhaba wa mahindi au watu wengine wakihitaji mahindi, yale mahindi yaliyokuwa yametengwa hayakuguswa kamwe. Wazazi hao walikuwa radhi mpunguze milo lakini siyo kutumia mahindi yale.
Hivi ndivyo wanavyofanya wakulima makini hata sasa. Jifunze kutoka kwa mkulima; ukivuna kipato chochote, weka kwanza pembeni 10%, tumia nyingine lakini hii 10% kamwe usiiguse. Hii ni mbegu ya kukuzalishia fedha zaidi hapo baadaye.
Fedha hii iweke sehemu ambayo itakuzalishia fedha nyingine zaidi mpaka mwenyewe utashangaa.
Kwa sasa unaweza kuiwekeza kwenye vipande, hisa au hatifungani.
Utajiri unajengwa kwa kujilipa wewe mwenyewe kwanza angalau 10% ya kila kipato chako kisha kuwekeza sehemu itakayozalisha zaidi.
Ni wakati wako sasa, ukipata fedha usitumie yote….wekeza sehemu ya hiyo fedha.
Akili ya akiba na uwekezaji ni miongoni mwa akili 6 zilizopo kwenye kitabu cha AKILI YA FEDHA. Jipatie nakala ya kitabu hiki muhimu kwako kujenga uhuru wako wa kifedha.
Habari njema ni kuwa unakipata kitabu hiki leo kwa bei ya ofa, sh 3,000 tu. Bonyeza kiunganishi hiki kujipatia kitabu hiki https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/85/
Au lipia sh 3,000 mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Utakipokea kitabu chako ndani ya dak 3.
"2025 Unastahili Zaidi Ya Ulichokipata 2024"
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899