Shauku 5 Zilizobeba Kusudi La Maisha Yako


Categories :

Rafiki! Kama kuna kitu kimoja unachotakiwa kwa namna yoyote ukitambue na kukiishi, basi ni kusudi la maisha yako.

Kusudi la maisha yako ndiyo sababu ya wewe kuletwa hapa duniani, mengine ni ziada tu.

Kati ya hasara ambayo mwanadamu huitengeneza, ni kuishi hapa duniani tena kwa muda mrefu lakini bila ya kuliishi kusudi lake kikamilifu.

Kumbuka mafanikio yako kamili, furaha yako kamili na utimilifu wako upo kwenye kuliishi kusudi lako kikamilifu.

Licha ya umuhimu mkubwa uliopo kwenye kuliishi kusudi,  watu wengi wanaondoka hapa duniani bila ya kuyaishi makusudi yao.

Hata wewe rafiki yangu utaondoka na kuiachia dunia hasara kama hutafanikiwa kulitambua na kuliishi kusudi lako kikamilifu.

Mojawapo ya sababu ya watu kutoishi makusudi yao ni kutokujua namna ya kutambua kisha kuishi makusudi yao kiukamilifu.

Moja na njia ya kulifahamu kusudi lako ni kuzipa  majibu shauku hizi tano zinazoweza kujitokeza maishani mwako.

1. Kitu kilichozidi njaa .
Moja nidhamu ambayo ni ngumu kuijenga ni nidhamu juu ya chakula. Imekuwa ni vigumu sana kujizuia kula chakula fulani au kiasi fulani kikubwa angali una fedha za kupata chakula hicho.

Kitu gani unapokifanya kinakufanya usahau kuwa kuna kula? Huko ndiko kwenye kusudi lako. Je ukianza kusoma au kuandika unasahau hadi kula? Ukianza kufundisha unasahau kama kuna kula?

2. Kitu kilichozidi starehe .
Kuna starehe nyingi duniani kwa sasa. Starehe zinaanzia kiganjani mwako. Simu kupitimia mitandao ya kijamii huamusha vichocheo vya kujisikia raha pale unapotumia. Hili limekuwa la kimbilio la watu wengi wanapotaka kukwepa kazi.

Je ni kitu unapokifanya kinakufanya usahau kabisa kuna starehe kwenye mitandao ya simu?

Kuna starehe nyingine kama kutoka ‘out’, kushabikia michezo,…Wewe ni sahabiki wa klabu ya  Simba au Yanga, je kazi gani utaendelea kuifanya hata kama Simba na Yanga watakuwa  wanacheza mechi?  Huko ndiko kusudi lako lilikojificha.

3. Tayari kusemwa na jamii.
Maoni ya watu yamekuwa mwiba kwa watu wengi kupiga hatua kubwa. Wapo waliowashirikisha wengine ndoto zao, lakini wakawaambia hawawezi kufanya vitu vikubwa kama hivyo, na wenyewe wakakubali.

Je ni kitu gani ambacho hata watu waseme haiwezekani wewe utawashanga?
Hicho ndicho kimebeba kusudi la maisha yako.

Rafiki yangu, hizi ni shauku 3 kati ya 5 ambazo ukizipa majibu zitakusogeza kwenye kulitambua kusudi lako.

Kitabu cha NGUVU YA KUSUDI kimesheheni mbinu nyingi za kukuwezesha wewe kutambua kusudi la maisha yako lakini na namna ya kuliishi kikamilifu ili kupata mafanikio makubwa unayostahili hapa duniani.

Hiki ni kitabu ulichotakiwa kuwa nacho tangu utotoni ili kujua kwa nini umezaliwa. Lakini kama muda huo haikuwezekana, muda mwingine ni leo, tena sasa.

Bei halisi ya kitabu hiki ni sh ~30,000~ , lakini kwa kutambua umuhimu wa wewe kutambua kusudi la maisha yako, leo utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa sh 5,000 tu.
Bonyeza kiunganishi hiki kujipatia kitabu chako https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/86/
Au wasiliana nasi kupiti 0752 206 899. Ofa hii ni ya leo tu.

"Hutasema umeishi duniani kama hujaishi sababu ya kuletwa duniani "

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer

AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *