Toka Tu Kwenye Mduara Huo Uone Maisha Yako Halisi


Categories :

Kama umekuwa ukikaa kwenye hali hii, ustarajie maajabu yoyote maishani mwako;

➢ Kutotaka kujisumbua.
➢ Kutotaka kujisukuma.
➢ Kutotaka kuumiza kichwa.
➢ Kutotaka kutoka kwenye mazoea.
➢ Kutotaka kujaribu.
➢ Kutotaka kuaibika.
➢ Kutotaka kukataliwa.
➢ Kutotaka kushindwa.
➢ Kukimbia hofu.
➢ Kufanya ulicho na uhakika tu.

Huku ni kung’ang’ania mazoea (comfort zone) ambayo hayana maajabu….

Je ungependa kuanza kupata matokeo makubwa unayostahili?

Basi hama mtaa wa “comfort zone” kisha hamia kwenye usahihi/upekee wako;

  1. Fanya kile unachoogopa  lakini chenye manufaa.
  2. Fanya kile ulichokiahirisha mara nyingi.
  3. Fanya kile kinachokupa maumivu.
  4. Fanya kile kitakachokuhitaji ufikiri zaidi. 5. Fanya kile kitakachokupa matokeo bora zaidi ya jana.
  5. Fanya kile kitakachokuonyesha upekee wako.
  6. Fanya kile kitakachokupa jina (Brand).
  7. Fanya kile ambacho hata ukifa dunia itaendelea kukuishi.
  8. Fanya kile kitakachokutoa jasho hata kama upo kwenye kiyoyozi. 
  9. Fanya kile ambacho kitahitaji fikra zako, uzingativu wako na hisia zako kuwepo pale.

Hizi ni kanuni za kukusaidia kutimiza malengo yako.

Bonyeza hapa kupata mwongozo wa kukusaidia kutimiza malengo yako; https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/70/

“Unastahili zaidi ya unachokipata sasa”

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer

AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *