Hakuna Muda Utajiona UpoTayari…..Wewe Anza…


Categories :

Hujafika ulikostahili kuwa kwa sababu kila ukitaka uanze safari….unajiona bado hujawa tayari.
[  ] Umekusanya na kula mtaji wa biashara mara nyingi sana, sasa anza biashara hiyo kwa mtaji huo mdogo…
[  ] Umekifikiri sana kitu hicho, sasa kiandike na kuanza kukifanya.
[  ] Umeahirisha sana kuonana na mtu muhimu ambaye atakusaidia kukusogeza mbele….kamuone leo.
[  ] Umesubiri sana kipato chako kiongezeke ndipo uanze kuweka,  anza kuwekeza hata 5% ya kila kipato chako.
[  ] Umeshasema  mara nyingi sana kuwa nitaanza kusoma vitabu , anza leo hata kurasa 5 kila siku..utaona mabadiliko.
[  ] Umecheza sana na malengo madogo, sasa ni wakati wa kuziendea ndoto zako kubwa.
[  ] Umesubiri matukio fualani ndipo uanze kufurahia maisha, wewe furahia kila siku.

Kama kuna muda ulikuwa unausubiria wa kufanya jambo zuri na muhimu maishani mwako, basi ni leo, tena SASA.

Anza LEO Anza SASA Anza n CHOCHOTE Ulichonacho.

Kujifunza zaidi juu ya kuamsha nguvu ya kujisukuma kuchukua hatua kisha kupata matokeo unayostahili,  bonyeza hapa https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/67/

“Unastahili zaidi ya unachokipata sasa”

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer

AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *