Ulizaliwa Unalia, Usikubali Ufe Ukilia Pia.

Wakati unazaliwa ni wewe pekee ulikuwa unalia angali mama yako na watu wengine wakitabasamu na kucheka.
Kuna kitu cha utofauti kinatakiwa kitokee wakati wa kufa. Wewe tu unatakiwa uwe unatabasamu kwenye jeneza angali watu wengine wakilia.
Watu watatakiwa walie kwa sababu wewe ulikuwa mkombozi wao kwani kuna thamani kubwa uliyokuwa unaitoa ambayo ilikuwa inatatua changamoto kubwa walizokuwa nazo.
Njia pekee ya kutoa thamani kubwa kwa wengine kiasi cha kuwaliza wengine unapokufa ni kuliishi kusudi lako kikamilifu.
Kama unatamani siku ya kufa kwako uwe pekee unayetabasamu wakati wengine wote wakilia, basi hakikisha unaishi kusudi la maisha yako kikamilifu. Kwani ndipo utagusa maisha ya watu wengine kiasi cha kutovumilia kutoa machozi watakapoona unaiaga dunia.
Kitabu cha NGUVU YA KUSUDI kinakusaidia wewe kutambua kusudi la maisha yako na kuliishi kikamilifu.
Kipate kitabu hiki sasa ili uanze kuishi sababu ya kuzaliwa kwako. Bonyeza hapa https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/86/
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899