Fedha Nyingi Zilipita Mikononi Mwake..Lakini Uzee ulimkaribia Angali Hana Fedha Yoyote Mfukoni Mwake.


Categories :

Abneri alitoa jasho jingi kuhakikisha anapata fedha mikononi mwake.

Alianza kupata sh 100,000 kila mwezi lakini baadye kipato chake kilikua na kufika zaidi ya milioni 2 kwa mwezi.

Lakini wakati wote kila kipato alichokipata alikitumia kwa kununua vitu ambavyo vilipoteza fedha yake kabisa…na vingine viliendelea kuchukua fedha yake mfukoni.

Alipofikisha miaka 50, Abneri alikaa chini na kupiga hesabu ya fedha zilizopita mikononi mwake. Alishangaa sana kuona kuna fedha nyingia sana zilipita mikononi mwake angalia hakuna fedha yoyote iliyokuwa imebaki mfukoni mwake.

Ndipo Abneri akakutana na nukuu hii kutoka kwa mwekezaji maarufu wa dunia, Warren Buffett “Kama hutatafuta namna ya fedha kuingia mfukoni mwako angali umelala, basi itakulazimu wewe kufanya kazi kwa ajili ya fedha mpaka unakufa.

Abneri alitambua kuwa kuna maarifa sahihi ya nini akifanye baada ya kupata fedha aliyakosa.

Kwa sasa humuambii kitu Abneri kwani kwenye kila fedha anayoipata lazima atenge 10% au zaidi na kuwekeza sehemu ambayo inamzalishia zaidi ya 12% kwa mwaka….

Na tayari kuna fedha zinaingia hata usiku akiwa amelala.

Abneri hakwenda kwa mganga kwani asingemsaidia bali alianza kujenga AKILI YA FEDHA ambayo imefanya mapinduzi makubwa kwenye maisha yake.

Inawezekana na wewe unapitia maisha ya Abneri aliyokuwa anatumia kila fedha. Wewe shituka mapema, anza kujenga akili ya fedha ikusaidie kuanza kufanya uwekezaji ambao siku itafika , hata usipofanya kazi lakini fedha zitakuwa zinaingia mfukoni mwako tu…..

Kujenga AKILI 6 MUHIMU ZA FEDHA, bonyeza hapa kupata mwongozo; https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/85/

” *Uhuru wa fedha ni haki yako, uujenge"*
Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer

AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *