Hivi Ndivyo Alivyofundishwa Kupata Chochote Alichotaka..

Kijana mmoja alimfuata mzee wa hekima na kumuuliza afanye nini ili aweze kupata kile anachokitaka maishani mwake?
Basi mzee wa hekima akamchukua kijana yule mpaka ufukweni kisha akaingia naye baharini kwa mtumbwi.
Walipofika eneo ambalo aliona lina kina kirefu, akamdondoshea yule kijana kwenye maji….ndipo yule kijana alianza kutapatapa kuzama majini kwa kuwa alikuwa hawezi kuogelea.
Mzee wa hekima alipoona yule kijana anataka kuzama, akawaita watu waliokuwa karibu wakivua samaki wamtoe majini na kumrudisha tena kwenye mtumbwa wake.
Mzee akaendesha mtumbwi tena mpaka ufukweni. Kijana yule alikuwa amechoka sana huku akimlalamikia yule mzee kuwa…nilikuja unifundishe namna ya kupata chochote ninachotaka, mbona wewe umekuja kuniua hapa?
Mzee wa hekima akajibu kuwa hili ndiyo lilikuwa somo lenyewe. Kisha mzee akamuuliza maswali yule kijana.
Je ulipokuwa unatapatapa ukijiokoa na kifo cha kuzama,
[ ] Je ulikuwa unawaza juu ya mifugo yako nyumbani? Kijana akasema HAPANA.
[ ] Je ulikuwa unawaza chakula ulichobakisha nyumbani. Kijana akasema HAPANA.
[ ] Je ulikuwa unawaza nguo nzuri ambayo ulikuwa bado hujaivaa. Kijana akasema HAPANA.
Ndipo yule mzee akamuuliza yule kijana, basi ulikuwa unawaza nini basi.
Kijana yule akasema kuna kitu kimoja tu nilikuwa nahangaika nacho muda huo….ni kupata hewa ili niendelee kuishi.
Vingine vyote havikuwa na nafasi yoyote kwangu.
Ndipo yule mzee wa busara akamuambia yule kijana, hili ndilo somo nililotaka kukufundisha.
Utakipata kitu chochote duniani kama utajenga shauku kubwa ya kukipata kitu hicho na kuziba masikio kwenye changamoto na fursa zitazokushawishi uachane na unachokitaka.
Kujenga shauku kubwa ni hatua mojawapo kati ya hatua 10 za kuchukua ili kutimiza malengo yako zilizopo kwenye kitabu cha MWONGOZO WA KUTIMIZA MALENGO YAKO.
Kipate kitabu hiki leo kikuongoze kupata ulichokitamani kwa siku nyingi. Habari njema ni kuwa leo utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa sh 3,000 tu.
Lipia mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika) au bonyeza hapa; https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/70/
Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899