Kama Unaanza Lakini Hufiki Mbali…Basi Hiki Ndicho Kinachokuzuia… 🔗


Categories :

Siku moja mbwa aliupata mfupa mkubwa wenye radha. Alifurahi sana kisha akauchukua ili atafute sehemu tulivu na kuufaidi vizuri. 🦴

Alipokuwa akivuka mto aliiona taswira yake ndani ya ya yale maji, alidhani ni mbwa mwingine amebeba mfupa.

Alipata wivu wa kutaka kumnyang’anya mbwa mwingine huo mfupa asijue ile ilikuwa taswira yake tu.

Alipoanza kubweka ili kumtisha huyo mbwa mwingine auachie mfupa, mdomo wake uliuachia  mfupa na ukaenda na maji na hakuupata tena.

Ulichoamua kukishikilia mwaka 2025 ni cha thamani kubwa sana kama utaendelea kukifanya kwa msimamo bila kuhangaika na vingine.

Hakikisha kila siku umefanya kitu kwa ajili ya jambo unaloamini litakufanya utoboe maishani.

🎯’Kufoksi’ ni moja kati ya hatua 10 za kukusaidia kutimiza malengo yako zilizopo kwenye kitabu cha MWONGOZO WA KUTIMIZA MALENGO YAKO.

Kipate kitabu hiki kiamshe na kuendeleza ndoto zako. Habari njema ni kuwa leo utakipata kwa bei ya ofa, sh 3,000 tu. Lipia mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika) na utakipokea ndani ya dak.3,
⤵️au bonyeza hapa kukipata sasa; https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/70/

Karibu sana .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *