Je Unaipeleka Kliniki Biashara Yako?
Baada ya mtoto kuzaliwa huanzishiwa kliniki ambapo hupelekwa kwevye vituo vya afya kila baada ya muda fulani, mara nyingi kila mwezi. Lengo la kumpeleka kliniki ni kutaka kujua maendeleo yake.
Baada ya mtoto kuzaliwa anategemewa atakuwa anakua; yaani kuongezeka uzito, kimo nk. Pia atakuwa anaonyesha kukua kiakili, viungo nk. Baada ya muda fulani anatarajiwa aanze kutambaa, kusimama, kutembea na kukimbia pia.
Kama maendeleo haya yasipoonekana, mtoto huyo hufikiriwa kuwa ana shida na hivyo hatua mahususi huchukuliwa ili kurekebisha hali hiyo. Hivi ndivyo inavyotakiwa kufanyika kwenye biashara yako ili iweze kukua na kufikia mafanikio makubwa. Lazima iwe na tabia ya kukua baada ya kuianzisha ili kufikia picha uliyonayo kwenye maono yako.
Kliniki ya mtoto hupima mtoto kwa vigezo maalumu. Moja ya kigezo hicho ni uzito(kg au gm). Kama mtoto ana afya njema namba hii hutarajiwa kuongezeka kadri muda unayokwenda. Kama namba hiyo haiongezeki kadri muda unavyoenda, huashiria kuna shida kwa mtoto.
Biashara pia inahitaji namba ili kutambua mwenendo wake. Ni kwa kupitia namba ndipo unapoweza kutambua maendeleo ya biashara yako. Kupitia namba za biashara utatambua kama biashara yako inatoa faida au laa. Ni kwa kupitia namba unajua biashara yako inauza kiasi gani na kila kitengo kinafanya kazi ufanisi gani.
Namba moja wapo ni mtaji unaozunguka. Hii ni kiasi cha fedha kinachozunguka kwenye biashara yako kwa ajili ya uendeshaji na uzalishaji. Kiasi hiki hakihusishi thamani ya mali ambazo zipo kwenye biashara yako kama magari, samani.nk. Mtaji unaozunguka ni namba muhimu sana kujua ni kiasi gani kinachochangia kwenye faida inayopatikana. Je kiongezwe au laa?
Namba nyingine ni faida. Lengo kuu la biashara yoyote ni kutengeneza faida. Kama biashara yako haitengenezi faida basi ujue inakufa. Kila wakati ipeleke kliniki biashara yako kujua kama ina uhai wa kutengeneza faida au la!
Kuna namba za biashara zaidi ya tano ambazo kama mfanyabiashara inabidi uzifahamu na uzitumie ili kujua mwelekeo wa biashara yako. Hizi ni namba ambazo kila biashara unayoiona imefanikiwa huzitumia kwa umanifu. Kwa nini na wewe usizitumie kwenye biashara yako ili kuifikisha biashara yako kwenye mafanikio makubwa?
Mtandao wa AmshUwezo upo tayari kukufundisha kuhusu Kliniki ya biashara yako. Hivyo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada “UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO”
Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kwa kina kabisa namba muhimu za biashara yako ili uweze kuzitumia na kuifikisha biashara yako kwenye mafanikio makubwa.
Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kisha kulitumia.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Biashara isiyo na Kliniki inajiandaa kufa. Usikise fursa hii muhimu ya kujua namba za biashara.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz