Haya Ndiyo Maamuzi Bora Ambayo Leo Utafanikiwa Kufayafanya.
Lengo kuu la kusimama mbele ya kioo cha kujitazamia huwa ni kujitazama na kujiona sehemu zile ambazo macho yako hazioni kirahisi. Hata kama uso ndio sehemu ambapo macho yako yapo lakini si rahisi kujiona. Hivyo kioo huwa msaada mkubwa sana kujiangalia uso kwani uso wa bianadamu ni kama mapokezi ya mtu anayekuangalia.
Lakini baada ya kujitazama inatarajiwa kama utaona kuna kasoro yoyote kwa mfano uchafua machoni basi uutoe na kuwa msafi. Hii ni kwa sababu kusimama kwenye kioo, kuuona uchafu bila kuutoa kutakuwa hakuna maana yoyote ya kwenda mbele ya kioo hicho ambacho ulitarajia kikukosoe.
Lakini watu wengi wamekuwa wakienda mbele ya kioo na kuuona uchafu wao lakini mwisho wa siku hawachukui uamuzi wa kuutoa uchafua huo. Inawezekana na wewe ni miongoni mwa watu hao. Utajiuliza ni lini na kwa namna gani? Kitendo cha kujua nini inabidi ufanye ili uweze kuboresha maisha yako lakini kutokwenda hatua inayofuata ya kufanya maamuzi ya kuweka vitendo ni sawa na kuuona uchafu machoni mbele ya kioo lakini kuacha kuchukua uamuzi.
Ni mara ngapi umetambua kuwa ili uweze kupata matokeo ya kitu unachokitaka ni lazima uweke kazi lakini hujafanya hivyo na hata pale ulipofanya ukaiishia njiani? Ni mara ngapi ulitambua kuwa ili uweze kupata fedha kwa ajili ya mtaji wa biashara huna budi kuweka kiasi fulani cha fedha kwenye kila kipato unachokipata lakini hujaanza kufanya hivyo?
Kanuni ya kwanza ya Newton ya mwendo inasema “Kitu kitaendelea kubaki katika hali yake ya utulivu kama hakutakuwa na nguvu yoyote kutoka nje itakayokifikia” Ndugu! hakuna kitu kinachoweza kutokea katika maisha yako kama hutachukua maamuzi ya kufanya. Matokeo yanatokeo kwa kuchukua hatua na si kuishia kutamani tu.
Moja ya uamuzi ambao unatakiwa uchukue maishani mwako ili uweze kufikia uhuru wa kifedha ni kuwa na baishara yenye mafanikio. Kuanzisha na kukuza biashara kisha kufikia mafanikio makubwa imekuwa changamoto kwa watu wengi. Watu wengi wameanzisha biashara lakini zimeishi kwa muda mfupi na kisha kufa na kuwaachia hasara kubwa. Wapo ambao wamekuwa wakiwaza kila siku ni kwa namna gani wanaweza kupata wazo bora la biashara. Haya yote yanajibiwa na mtandao wa AmshaUwezo.
Mtandao huu umekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada ya semina hii ni UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kiundani namna ya kupata wazo na kuweza kuanzisha biashara kisha kuikuza na kufikia mafanikio makubwa. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.
Tumeona hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako bila kufanya maamuzi na kuchukua hatua sahihi. Ni wakati sasa umekufika wa kufanya maamuzi sahihi. Kama kweli unataka kuboresha kipato chako usifikirie kuikosa semina hii. Fanya maamuzi leo kwa kujiunga kupitia kiunganisha hapo chini.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Haya ni maamuzi sahihi na muhimu sana ya kuchukua mwaka huu. Usipange kukosa nafsi hii, jiunge leo.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz