Shikilia Tochi Yako


Categories :

“Huhitaji mwanga wa mwezi uangaze nchi nzima ili uione njia yako ya kupita usiku. Mwanga wa tochi ulioishikilia mkononi bila kuiachia inaweza ikakuongoza njia na kufika uendako”

 Kama unatembea usiku, mwanga wa tochi utatosha kumulika  njia unayoipitia na kufika unakoenda. Huhitaji mwezi umulike nchi nzima ndipo uweze kupita.

Katika maisha yako huhitaji kuwa na kila kitu ndipo uishi maisha yako ya utoshelevu. Huhitaji  kuwa na kila aina ya kipaji ndipo uweze kufanya makubwa.  Huhitaji kuwa na kila taaluma ndipo upate kufanya makubwa yenye miujiza.

Maishani unahitaji kufanya jambo moja au machache kwa viwango vya juu kukufikisha kwenye mafanikio makubwa. Chagua jambo moja ambalo unalipenda kulifanya na lifanye kwa viwango vya juu sana. Utaweza kupata mafanikio makubwa kwa kujikita na kupanga malengo makubwa kupata matokeo makubwa. 

Tumeshuhudia wanamichezo kama Christian Ronaldo au Lionel Messi akijikita kufanya mipra wa miguu kwa kiwango cha juu sana. Lakini hao wawili wana mafanikio makubwa kwa kuchagua kufanya mpira tu. Mwangalie Warren Buffett aliyeamua kujikita kwenye uwekezaji, amepata utajiri mkubwa na kuwa miongoni mwa matajiri kumi wa juu kwenye orodha ya matajiri duniani.

Kupata mafanikio makubwa hakukuhitaji uwe na vipaji vingi, kipaji kimoja tu kinaweza kukuwezesha kutimiza kusudi na ndoto zako. Kipaji cha kuongea kwa ufanishi tu kinaweza kukuwezesha kufikia umaarufu  mkubwa . Kipaji chako cha kuchekesha tu kinaweza kikakufikisha. Kipaji chako cha ushauri ukikifanya kwa kiwango kikubwa kitakufikisha kwenye safri yako ya mafanikio. Kipaji chako cha cha kushawishi watu kinaweza kikakufanya kuwa  muuzaji mzuri na kupata mafanikio makubwa.

Huhitaji kufahamu kila kitu ndipo uanze kukifnya kitu hicho. Pata maarifa ya kuanzia kisha anza na utakuwa unaendelea kujifunza kadri unavyoendelea kufanyia kazi vile ulivyovianza. Watu wengi wamekwamia hapo, kila wakitaka kuanzisha vitu, wanahisi kuna kitu wanahitaji kujifuanza zaidi na mwisho wa siku wameshindwa kaunzsiaha kabisa. Hakuna siku ambayo utakuwa unajua kila kitu na ukajiona upo tayari washa tochi ya maarifa uliyoanayo kisha anza safari yako.

Anza biashara na mtaji mdogo ulionao. Siku nikipata mtaji ndipo nitaanzisha biashara ya ndoto yangu; mwaka na miaka inapita bado hujaanzisha biashara yako. Kwani kwani una kiasi gani mkononi mwako? Je hicho kiasi ulichonacho huwezi ukafanya kitu kwa ajili ya biashara yako? Mbona ulikusanya kiasi baadaye ukakitumia chote! Tafakari vizuri kiasi ulichonacho kinaweza kufanya jambo fulani kwenye biashara unayotaka kuianzisha, kitumie kama tochi kumulika njia ya safari yako.

Ndugu wakati umefika sasa wa kuanza safari yako ya kutengeneza mafanikio yako kwa kutumia hata hicho kimoja unachokiona. Kaa chini na tafakari; ni kipaji gani unacho? una mtaji kiasi gani?kitu gani unaweza kuanza kukifanya? Usiendelee kusubiri mpaka mwezi umulike ndipo uanze safari yako, tochi uliyonayo mkononi inakutosha kumulika njia unayotaka kupita na kuendelea na safari.

Hivyo ulivyonavyo sasa na hapo ulipo panakutosha kuianza safari na kuendelea kujenga na kukua kadri muda unavyokwenda. Biashara gani unaanza kuijenga sasa? Kipaji gani unaanza kukikuza sasa? Mahusiano gani unaanza kuyatengeneza leo? Nidhamu gani unaanza kuijenga leo? Kiasia gani cha akiba unaanza kukiweka leo? Usisubiri vikubwa anza na hicho kidogo.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,

Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),

Mawasiliano;

Simu; 0752206899/0714301952

Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *