Washa Njiti Ya Maisha Yako


Categories :

“Njiti ya kiberiti ina uwezo wa kuteketeza mamilioni ya hekta za misitu iliyounganishwa pamoja”

Ukiangalia njiti ya kiberiti unaweza ukaidaharau sana na kuoana si chochote. Lakini njiti ya kiberiti ndiyo inayoanzisha moto na kuchochesha kiasi cha kuivisha tofari na hata kupasua miamba. Kadhalika njiti hiyo ina uwezo wa kuteketeza misitu ya mamilioni ya miti kama imeungana pamoja.

Una njiti katika maisha yako inayoweza kuwasha moto kwenye maisha yako na kukupa mafanikio makubwa. Njiti hiyo ni wazo. Wazo moja tu linaweza kubadilisha kabisa taswira ya maisha yako. Wazo moja tu la biashara linaweza kukupeleke kwenye utajiri. Wazo moja tu linaweza kubadili tatizo kubwa kuwa fursa.

Hatua zozote unazochukua ni kwa sababu ya mawazo unayoyatengeneza. Kama hatua unazochukua ni mbovu tambua kuwa chanzo chake pia kitakuwa kibovu hivyo huna budi kukibadili chanzo ili kuboresha hatua hizo.

Matokeo makubwa unayoyaoona hapa duniani ni kwa sababu ya mawazo ambayo watu waliyatengeneza na kisha kuyatumia. Kwa hiyo kama unajiona hujafanikiwa kufanya mambo makubwa katika maisha yako, basi tambua ni kwa sababu hujafanikiwa kuwaza vizuri na kutoa mawazo makubwa kisha kuyafanyia kazi.

Utajiri mkubwa unaouona ni kwa sababu ya mawazo ya kitajiri ambayo watu walifanikiwa. Mawazo ndiyo mbegu ya utajiri. Kwa kupitia wazo sahihi ndipo unapopata fursa ya kuwa na thamani kwa watu wengine. Kadri thamani hiyo inavyokuwa kubwa ndiyo watu watakuwa tayari kukulipa kiwango kikubwa na kukuwezesha kuwa tajiri.

Watu wengi wameshindwa kubadili maisha yao kwa sababu kuwaza ni kazi ngumu. Henry Ford alisema
“Thinking is the hardest work there is, which is probably the reason so few engage in it.” akimaanisha kuwa kufikiri ni kazi ngumu sana ndiyo maana ni watu wachache tu wanaifanya. Hii inaweza kuwa sababu kubwa ya kwa nini watu wachache tu ndiyo wanafanikiwa; watu wachache tu ndiyo wanaofikiri na kuja na mawazo sahihi ya kitajiri.

Ndugu! Mwanzo wako wa mafanikio upo kufikiri tena kufikiri kwa usahihi. Kwa sababu hii ni kazi ngumu lakini muhimu sana. Huna budi kulipa kipaombele jambo hili.

Unahitaji muda mzuri wa kufanya jambo hili. Asubuhi ndiyo muda mzuri kwa sababu ya utulivu unaoweza kupatikana. Usichelewe, kukicha utakutana na kelele nyingi. Tenga eneo maalumu ambalo utapata utulivu na kuweza kufikiri kwa kina. Muda wa kufikiri ukifika, jitenganishe na kelele za dunia, usitumie simu wala kuwa karibu na sauti nyingine zozote.

Soma vitabu mbalimbali. Tembea maeneo mablimbali. Huko utapata wazo ambalo ukianza kulifanyia kazi litabadilisha kabisa taswira ya maisha yako. Ili uweze kuokota fedha huna budi kutoka nje na kuwaza. Ukitaka kupata wazo nzuri jisukume kufikiri.

”Washa njiti ya mawazo yako, yanauwezo wa kuteketeza umasikini”

Hii ni Habari Njema Kwako!

Maarifa mazuri uliyoyapata hapo juu ni dondoo moja tu kati ya dondoo 366 zilizopo kwenye kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Hizi ni dondoo zilizojitosheleza kiasi cha kusoma dondoo moja na kupata hatua ya kuchukua na kwenda kufanyia kazi.

Kitabu hiki kinakupa nafasi ya kujenga nguzo za mafanikio katika maisha yako; nguzo hizo ni kama kutambua kusudi lako, uwezo na upekee wako, kuwa na maono, kuweka malengo na kujenga nidhamu ya kuyatimiza, kujenga uvumilivu na ustahimilivu ili kushinda vipindi vigumu vya maisha yako nk

Pata picha hiyo ni dondoo moja tu, je ukizipata dondoo zote 366 na kuchukua hatua utakuwa wapi mwisho wa mwaka? Naamini utakuwa mbali sana. Gharama ya kitabu hiki ni Sh 20,000/ lakini kwa sababu najali mafanikio yako, sasa utakipata kwa sh 15,000/ tu. Wahi kabla ya ofa hii kuisha. Wasiliana nami kupitia namba 0752 206 899(Alfred Mwanyika).

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *