Usitafute Miguu, Anza Kutembea.


Categories :



“Kama nyoka angejitazama kwanza na kuamini hana miguu asingeweza kuchukua hatua na kukimbia kwa kasi kuliko jongoo mwenye miguu mingi”

Kama ni suala la kutafuta visingizio na kushindwa kufanya chochote, basi nyoka angekuwa wa kwanza kuleta visingizio ambavyo vinaonekana wazi na ni vya kweli. Nyoka hana miguu, lakini hakutaka kuchukua hilo kama sababu ya yeye kutokutembea. Lakini yeye alichoamini ndani yake anaweza kutembea tena kukimbia kabisa.

Moja ya sababu ambayo imekufanya kufika hapo ulipo leo ni kwa sababu ya kuendelea kujitazama na kuona kuwa huna miguu na hivyo huwezi kutembea.

Umejitazama na kuona huna miguu ya uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa. Umejitazama na kuona huna miguu ya kipaji na hivyo huwezi kufanya kitu cha kipekee. Umejitazama na kuona wewe huna vitu vizuri walivyonavyo wengine na hivyo umeishia kujidharau. Hivyo kazi yako imekuwa ni kujiangalia nini huna na sio nini ukifanye.

Hizi zimekuwa sababu tu za kukuchelewesha kuchukua hatua na kufika unakotakiwa kufika. Kila ukijichukunguza unaona bado unahitaji maandalizi zaidi kuanza jambo. Kila wakati umejiona bado unahitaji muda wa kujianda kuchukua maamuzi, bahati mbaya miaka inaenda lakini bado unaona unahitaji muda zaidi wa kujiandaa.


Umejiangalia umeona huna miguu ya uwezo mkubwa wa kufanya miujiza. Baada ya kuangalia mafanikio makubwa ambayo watu wachache sana wameyapata, umejiona wewe huna uwezo huo wa kufanya mambo makubwa. Lakini hii ni habari njema kwako; una nguvu kubwa ndani yako hata kama hujaiona. Nguvu hiyo imelala tu ndani yako ikisubiri uiamushe na kuweza kufanya mambo makubwa. Ili kuifaidi nguvu hii kwanza amini kuwa ipo kisha anza kuweka malengo makubwa zaidi na kuweka nidhamu kubwa ya kuyafikia, hakika utaanza kupata matokeo makubwa kuliko sasa.

Ulipoangalia miguu ya vipaji umejiona wewe huna hata mmoja. Kipaji ni ujuzi au nguvu ya kipekee ambayo kila mtu anayo ndani yake. Hakuna mtu aliyependelewa hata wewe una nguvu hiyo. Kaa chini na tafakari ni vitu gani unaweza kufanya kirahisi kuliko watu wengine? Ni vitu gani unapenda kuvifanya? Anza kuviwekea mpango wa kuviboresha vitu hivyo. Anza kunoa kipaji hicho ili kiweze kukupa matokeo makubwa zaidi.

Ulipoangalia ulivyonavyo umejiambia huwezi kuwa na biashara. Umeangalia mtaji wako umeona huwezi kuanza biashara. Miaka nenda miaka rudi umeendelea kujiandaa na mtaji wa biashara na hujafanikiwa kuifungua mpaka leo. Anza na hicho ulichonacho, anzia hapo ulipo. Ukifanikiwa kuianza biashara hiyo utapata fursa ya kuikuza kuliko kuendelea kujiandaa.

Ndugu! Umekuwa ukiahirisha na kusingizia kuwa huwezi kufanya jambo fulani kwa sababu huna uwezo huo. Huo ni mtazamo tu lakini uwezo huo upo ndani yako. Kama ambavyo usivyoiona miguu ya nyoka, ndivyo na wewe unaweza usiuone uwezo huo mpaka utakapoamini unao na kuanza kuutumia. Anzisha biashara sasa, umeamini vya kutosha kuwa wewe huna uwezo huo. Ukianzisha ndipo utakapokutambua na nguvu kubwa ndani yako.


Hii ni Habari Njema Kwako!

Maarifa mazuri uliyoyapata hapo juu ni dondoo moja tu kati ya dondoo 366 zilizopo kwenye kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Hizi ni dondoo zilizojitosheleza kiasi cha kusoma dondoo moja na kupata hatua ya kuchukua na kwenda kufanyia kazi.

Kitabu hiki kinakupa nafasi ya kujenga nguzo za mafanikio katika maisha yako; nguzo hizo ni kama kutambua kusudi lako, uwezo na upekee wako, kuwa na maono, kuweka malengo na kujenga nidhamu ya kuyatimiza, kujenga uvumilivu na ustahimilivu ili kushinda vipindi vigumu vya maisha yako nk

Pata picha hiyo ni dondoo moja tu, je ukizipata dondoo zote 366 na kuchukua hatua utakuwa wapi mwisho wa mwaka? Naamini utakuwa mbali sana. Gharama ya kitabu hiki ni Sh 20,000/ lakini kwa sababu najali mafanikio yako, sasa utakipata kwa sh 15,000/ tu. Wahi kabla ya ofa hii kuisha. Wasiliana nami kupitia namba 0752 206 899(Alfred Mwanyika).

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *