Huwezi Kufika Safari Yako Kwa kuangalia ‘side mirror’ Pekee.


Categories :

Hata kama wewe siyo dreva wa gari lakini naamini umeshawahi kupanda gari lenye vioo vingi vinavyomsaidia dreva kuangalia maeneno mbalimbali akiwa barabarani. Vioo mojawapo ni vile vidogo, na vipo pembeni na mbele ya gari. Vioo hivyo vina jina maarufu la ‘side mirror ‘.

Kazi ya vioo hivi ni kumsaidia dreva kuangalia nyuma alikotoka. Kwa kuwa na uwezo wa kuangalia nyuma dreva huweza kujua gari linalokuja nyuma yake na kufanya mawasiliano kwa ajili ya usalama. Lakini pia humsaidia dreva kuona nyuma anapokuwa analirudisha gari nyuma.

Lakini licha ya umuhimu wa side mirror, dreva hawezi kufika safari yako kama macho yake yatakuwa yanaangalia kwenye side mirror tu. Kwa kufanya hivyo atapoteza uelekeo wa mbele. Hivi ndivyo ambavyo umekuwa ukifanya katika maisha yako. Umekuwa ‘busy’ na kuangalia side mirror badala ya kioo kingine kikubwa cha kukupa ueleke sahihi wa njia unayoiendea na kufika safari yako.

Uatakuwa unajiuliza ni kwa namna gani umekuwa busy kuangalia kwenye side mirror tu? Kwa kuendelea kuangalia makosa uliyotenda au vitu ulivyokwisha kupata badala ya kuweka mipango na jitihada za kusonga mbele, imekuwa sawa tu na dreva anacheza na side mirror tu bila kutazama kioo kikubwa kilicho mbele yake ambacho kingemuwezesha kuona eneo kubwa la mbele na kuiongoza gari lake kufika mwisho.

Ulichokosa. Kutumia muda mwingi sana kutafakari na kujilaumu kwa kile ulichokosa, ni kupoteza mwelekeo wa mbele. Hakuna mtu asiyekosea, lakini wanaofanikiwa ni wale wanaojifunza haraka kutoka kwenye makosa waliyofanya kisha kusonga mbele wakiwa bora. Hawatumii muda mwingi kulia kwa kile walichokikosea.

Ambacho huna. Je umekuwa ukitumia muda mwingi sana kutafakari na kusikitika kwa kile ambacho huna? Huku ni kuwa busy na side mirror na si kioo cha mbele. Hakuna mtu ambaye ana kila kitu. Hakuna mtu ambaye anafahamu kila kitu. Lakini kuna uwezekano wa kupata vingi. Lakini hakuna mtu ambaye hana chochote. Kama ni uwezo wa kufanya mambo kila mtu ana uwezo fulani maalumu wa kufanya vitu kwa utofauti. Hivyo badala ya kutumia muda mwingi kutawama kile ambacho huna, angalia ulichonacho kisha anza kukitumia hicho wakati ukiendelea kutafuta kile amabcho huna.

Mafaniko yako ya sasa. Hongera kwa mafanikio yako ya sasa, unastahili pongezi. Lakini usiyatumie mafanikio hayo kama side mirror kubakia ulipo. Mafanikio ya sasa imekuwa sumu ya mafanikio makubwa anayostahili mtu. Ukiyapata mafaniko shukuru, jipongeze kisha tumia mafanikio hayo kama ngazi ya kwendea mbele. Kama ni faida, basi geuza sehemu ya faida hiyo kuwa mtaji wa kupata faida kubwa zaidi.

Kuiga kwa jirani. Kama dreva atakuwa anaangalia kwenye side mirror kisha kumuiga dreva wa nyuma kuendesha gari lake, ni rahisi sana kupata ajali na kushindwa kufika mwisho wa safari yake. Unaweza kujifunza kutoka kwa jirani lakini usiige kila kitu utapotea.

Kutokuwa na ndoto. Mtu aliye na ndoto huona anakoelekea na njia atakazopitia hata kabla hajafika huko. Hivyo mawazo yake huwa mbele kila wakati. Hana muda wa kupoteza kungalia alikoanguka na kuendelea kujilaumu. Kutokuwa na ndoto kunakufanya ujikite kuangalia ulikotoka na hapo ulipo tu.

Ni kweli umeanguka lakini Usiendelee kulala hapo, inuka nenda mbele. Umepata mafanikio, hongera lakini yatumie kama ngazi ya kufanya makubwa zaidi. Jenga ndoto yako; nini unataka kupata maishani mwako. Hicho kitakuwa kioo chako cha kuangalia mbele kila wakati.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *