Hii Ndiyo Njia Pekee Ambayo Wengi Wamepiga Hatua Kubwa Kupitia Maarifa.


Categories :

Wapo wachache walionufaika na maarifa, lakini wengi wakishindwa kutumia fursa hii katika kuishi maisha ya mafanikio. Huwezi kutenganisha mafanikio unayoyataka na maarifa. Kila utakachopanga kukifanya ili kupata mafanikio, kina changamoto zake hivyo kuhitaji majibu ili kuweza kuzitatua na kisha kusonga mbele.

Changamoto nyingi ambazo mtu anakutana nazo na kisha kumkwamisha kusonga mbele, ziliwakumba watu wengine pia. Wale waliokutana nazo awali, wengine walizitatua na njia za utatuzi walihifadhi kwenye vitabu, sauti, nk. Wapo waliofanya majaribio mbalimbali ili kujua njia nzuri ya kufanya jambo fulani. Hivyo tatuzi za changamoto nyingi zinazowakumba watu sasa, zilisha patiwa majibu

Oh! Kumbe majibu ya mtihani unaoufanya yapo halafu bado unafeli!

Linapokuja kwenye matumizi ya maarifa kama chachu ya mafanikio, kuna makundi yafuatayo ya watu;

Wapo ambao hawajui kama kuna maarifa. Hili ni kundi kubwa sana la watu ambalo tunalo hata kwenye nchi zetu za kiafrika. Watu hawa hawajui inabidi wasome vitabu ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili.

Kundi la pili ni wale wanaoatambua kuwa kuna maarifa lakini hawaamini kwenye maarifa hayo. Hili pia ni kundi kubwa la watu. Watu hawa hawaamini kama kuna uhusiano wowote kati ya mafanikio na maarifa. Hivyo hata kama atakikuta kitabu ambacho maudhui yanamlenga yeye moja kwa moja, hatakubali akifungue kwa sababu hata imani hiyo. Hii ndiyo sababu ya kuwa na msemo huu “Ukitaka umfiche kitu mwaafrika basi weka kwenye kitabu”

Kundi la tatu ni la wale wawanaoamini kuwa kusoma au kuatafuta maarifa ni kipaji. Mimi sina kipaji cha usomaji! Kuna watu wenye vipaji vyao vya kusoma. Hivyo wamewaachia wachache watafute maarifa. Hawa ni wale ambao kama ni kitabu atakisoma kidogo na kuacha kwa sababu anajiona hana kipaji hicho.

Kundi nne ni wale wapata maarifa lakini hayawasaidii. Hili ni kundi ambalo watu huweka juhudi kuyapata maarifa na kuhamasika bila kuchukua hatua au kuchukua hatua kisha kuishia njiani. Hawa wanapata hamasa ya mshumaa ambapo kadri muda unavyoenda huendelea kuungua huku ukipungua hivyo na hamasa hiyo huzidi kupoa kadri muda unavyoenda.

Kundi la tano ni wale wanaoamini kuwa maarifa ni mafanikio. Hawa hupata maarifa na bila kuchelewa huweka maarifa hayo kwenye matendo. Baada ya kuweka kwenye matendo, hupata matokeo bora zaidi ya mara yale waliyokuwa wamezoea kupata. Hii huwa hamasa kwake ya kuendelea kutafuta maarifa zaidi na kuyatumia.

Kundi hili limeweza kupata faida ya taaluma za watu wengine hata walio mbali. Wanaendelea kupata maarifa bila kuridhika na hivyo kuwa na hamasa ya kuchukua hatua bila kukoma. Hawa ndiyo wanaofanikiwa kuamsha uwezo wao na kupata mafanikio makubwa wanayostahili.

Ushauri wangu kwako.

Nakuomba ujiunge na kundi la tano. Ukishapata maarifa jisukume kutumia na kupata matokeo. Utakapopata matokeo itakuhamasisha kuendelea kusaka na kutumia maarifa. Hii itakuwa njia pekee ya wewe kutenda muujiza kwa maarifa unayoyapata mara jwa mara.

Kutabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni kitabu kilichojaa maarifa mzuri kuhusu hazina uliyonayo ndani yako; uwezo. Mwishoni mwa kila sura kuna hatua kadhaa za kuchukua na kuweza kuamsha uwezo wako na kupiga hatua kubwa zaidi. Jipatie nakala yako leo na uanze kunufaika na maarifa. Bei ya kitabu hiki ni sh 15,000/ Lakini leo utakipata kwa bei ya promosheni ya sh 10,000/. Hii yote ni kuhakikisha unaanza kunufaika na maarifa sahihi. Wasiliana nami kupitia 0752 206 899.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *