Huyu Ndiye Anayekukwamisha Usifanikiwe! Mkamate Leo!


Categories :

Ukienda mbele ya kioo cha kujitazamia, atakayekuwa anaonekana kwenye kioo hicho ni yule aliyesimama mbele ya kioo hicho. Miongoni mwa watu hao atakuwa ni wewe. Kwa hiyo kama akisimama pekeyako utaonekana pekeyako.

Itakuwa ajabu kama utasimama mbele ya kioo ukaiona taswira moja tu kwenye kisha ukaanza kutafuta ni nani aliyesimama kwenye kioo hicho!

Umepata hamasa kubwa ya kujua nani anayekwamisha wewe kufanikiwa. Lakini nasikitika kukuwambia kuwa wewe ndiye uliyesimama mbele ya kioo, na kuna taswira moja tu kwenye kioo, bado unatafuta nani alisababisha taswira hiyo.

Kama mtu amefanikiwa mtu wa kwanza kuulizwa kuhusu kufanikiwa kwake ni yeye mwenyewe aliyefanikiwa. Vivo hivyo kama ameshindwa katika maisha yake mtu wa kwanza kuulizwa ni yeye mwenyewe aliyeshindwa.

Hivyo mtu pekee aliyesababisha wewe kushindwa ni WEWE MWENYEWE. Leo umkamate akueleze vizuri kwa nini amesababisha wewe kushindwa. Hata kama utakuwa na orodha ndefu ya watu ambao unafikiri wamesababisha wewe kushindwa, basi jina la kwanza kutokea kwenye hiyo orodha inatakiwa liwe lako.

Umeacha kuwa wewe. Licha ya dunia kuwa na zaidi ya watu bilioni nane na Tanzania kuwa na watu zaidi ya milioni sitini sasa, WEWE upo mmoja tu hapa duniani. Hivyo unatarajiwa kufanya vitu vya kipekee kulingana na upekee ulionao. Lakini kwa kutotambua upekee wako na kuwa mtu yoyote, umeamua umesjisababishia kutofanikiwa kikamilifu. Tambua leo ni kitu gani unaweza kufanya kwa ubora mkubwa kuliko wengine? Fanya hicho na acha kuiga.

Unajua cha kufanya lakini unafanye kingine. Unatambua kuwa huwezi kupata matokeo kama utakuwa unaahirisha lakini bado unaahirisha na unatarjia mabadiliko yoyote! Unafahamu kuwa ili uwe na siku nzuri na bora ni lazima uamke mapema, lakini hufanyi hivyo. Huko ni kujikwamisha mwenyewe.

Umewalalamikia wengine wewe umejitoa. Kwenye kila baya au kushindwa kwako, umemtafuta mtu wa kumlalamikia. Umeilalamikia serikali kwa hali yako mbaya ya uchumi hata kama wewe unatoa thamani ndogo au hakuna wa watu wengine. Umelalamika kuwa wengine hawakujali wakati wewe mwenyewe hujijali. Je unajipenda hata kama mtu mwingine hajasema? Je unajiamini hata kama watu wengine hawaonyeshi hilo?

Hujaanza kuishi japo unaamuka kila siku asubuhi. Licha ya kuwa ni muda mrefu tangu umezaliwa lakini hujaanza kuishi mpaka leo. Kila siku unasema nikipata hiki ndipo nitafurahi sana, hata ulipkipata furaha yako ilidumu kwa muda mfupi. Baada ya hapo ukaweka kigezo kingine. Ndugu maisha yako ni muda, muda wako wa kuishi hapa duniani ukiisha ndiyo basi. Kama kuna kitu unatamani kukifanya muda mzuri ni leo tena sasa. Anza kutekeleza mipango uliyoifikiri kwa muda mrefu. Aza kuishi, usiahirishe kuishi.

Unaweka malengo lakini huyatimizi. Umekuwa mwaminifu sana kila mwanzo mwa mwaka kuweka malengo ya kufanyia kazi. Sahuku imekuwa kubwa sana mwanzoni mwa mwaka lakini imepoa kabisa baada ya miezi miwili tu! Ukiulizwa leo malengo yako uliyoweka Januari hukumbuki hata moja. Hujafanya uliyopanga lakini unataka matokeo ya yale uliyopanga. Wewe ndiye mkwamishaji wa kwanza wa mafanikio yako.

Ndugu! Umemuona mtu wako ambaye amekuwa akikuzuia kila siku kufanikiwa ni wewe mwenyewe. Kumbe kama utaamua kubadilika kwa hujitambua wewe sahihi, kuchukua jukumu la maisha yako, kuweka nidhamu kubwa kisha kuanza kuishi leo. Utafanikiwa sana. Anza leo.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *