*Kuna Mapinduzi Makubwa Sana Yatatokea Kwenye Maisha Yako! Anza Kutumia Neno Hili….. Tu


Categories :

Ni tamanio la watu wengi kutaka kufanya makubwa. Karibu kila mtu utakayemuuliza kama anataka kufanikiwa katika maisha yake atasema ndiyo.

Licha ya matamanio hayo, wengi wameshindwa kupata mafanikio hayo. Lakini wapo ambao wapo ”bise” sana lakini bado hawafikii hata nusu ya matokeo wanayoyatarajia. Lakini wapo ambao hawajafikia mafanikio hayo wakisingizia mambo ni mengi muda ni mchache.

Lakini waliofanikiwa na walioshindwa wote wana saa 24 kwenye wiki na siku saba kwenye juma. Sasa ukisema wewe una muda mfupi, jiulize ni nani aliyeongezewa hata sekunde moja?

Kuna kitu kimoja ambacho hao waliofanikiwa wanafanya licha ya kuwa na muda sawa na wewe. Kitu hicho ni matumizi ya neno HAPANA. Kuna mapinduzi makubwa pia yatatokeo kama na wewe utaanza kulitumia neno hili.

Watu wengi hawapendi na wanaogopa kutumia neno hapana. Wanaogopa kusema hapana kwa watu wao wa karibu hata kama walichoambiwa wafanye hawakipendi. Wanaona wakiwakatalia watajisikia vibaya. Kwa kufanya hivyo wanakuwa na mambo mengi ya kufanya kiasi cha kushindwa kufanya mambo muhimu kwenye maisha yao.

Sema HAPANA kwenye tabia zako za kushindwa. Maisha ya mafanikio yanatokana na kuishi tabia za mafanikio. Ni mpaka useme hapana kwenye tabia za kushindwa ndipo utaweza kuishi tabia hizi za mafanikio. Sema hapana kwenye uvivu, kutowajibika, kulaumu nk. Hii ni kusema hapana kwako mwenyewe wakati tabia hizi zinapokunyemelea.

Sema HAPANA kwenye mambo ambayo hayapo kwenye ratiba. Unaamuka asubuhi ukiwa umepanga ratiba kabisa kuwa leo nitafanya moja, mbili, tatu, je ndiyo unayoyafanya? Au jambo jingine lolote likijitokeza linapewa nafasi? Ili uweze kufanya mambo muhimu yaliyopo kwenye ratiba lazima useme hapana kwenye mambo mengine ambayo hayakuwa kwenye mpango.

Sema HAPANA kwa watu wasiokufaa. Watu wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana kwenye hatua unazachukua. Umekuwa nao kwa muda kwa mrefu sasa, je wamchangia wewe kupiga hatua? Kama jibu ni hapana ni vizuri kusema hapana kwao kisha kusema ndiyo kwa wale wanoakwenda kwenye uelekeo wako.

Sema HAPANA kuwa mtu mwingine. Wewe ni mtu wa pekee uliumbwa kwa namna ya pekee na kuwekewa uwezo wa kipekee ndani yako. Kuna vitu unaweza kuvifanya wewe tu tena kwa kiwango cha juu sana. Je umeshaionyesha dunia vitu hivyo. Kama jibu ni hapana, ina maana kuwa hujaanza kuishi wewe wa kipekee na badala yake umeangalia tu mtu mwingine anavyoishi kisha kumuiga. Umepoteza upekee wako. Sema hapana kuwa mtu mwingine kisha anza kuishi upekee wako.

Ndugu! Mafanikio yako yatapatikana utakapoanza kutumia neno hapana kwa ujasiri. Ukianza kutumia neno hili utafanikiwa kuishi upekee wako. Utaweza kuishi maisha yenye matokeo makubwa pale utakapoacha kuiga kisha kuishi upekee wako na kuamsha nguvu yako ya kipekee ndani.

Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI HALISI kimeeleza kiundani kuhusu kuibua upekee wako kisha kuamsha nguvu yako ya kipekee. Kama kweli unataka mafanikio makubwa uliyoyaota kwa siku nyingi hakikisha umekipata kitabu hiki. Gharama ya kitabu hiki ni sh 15,000/ lakini kwa sababu nakujali wewe rafiki yangu, nitakuuzia kwa sh 10,000/ ili ukipate na kuanza kuishi maisha unayostahili. Karibu ujipatie kitabu chako kabla ofa haijaisha. Mawasiliano: 0752 206 899. Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *