Kwa Nini Wewe Hupati Licha Ya Dunia Kuwa Na Utele ?


Categories :

Moja ya sifa nzuri ya dunia ambayo kila mtu angependa kuisikia ni hii; dunia ina utele.

Ni kweli dunia ina utele. Neno utele linamaanisha vitu vingi visivyoisha. Kuna viashiria vingi vinavyoonyesha utele wa dunia.

Kwa mfano dunia ina zaidi ya watu bilioni nane kwa sasa. Watu wote hawa wanahitaji hewa safi ili waendelee kuishi. Lakini licha ya uhitaji huu mkubwa, dunia haijawahi kuishiwa hewa hiyo kiasi cha watu kuanza kugombaniana.

Kadhalika licha ya wavuvi kuendelea kuvua samaki kwenye maziwa na bahari kwa miaka mingi, lakini maziwa na vahari havijawahi kuishiwa samaki. Huu ni utele.

Utele huu unaenda mpaka kwenye vitu vingine ambavyo mwanadamu angetamani avipate kama vile utajiri, afya, mahusiano mazuri, umaarufu, na mafanikio mengine.

Swali linakuja, kama kuna utele kwenye mafanikio, kwa nini watu hawajafanikiwa? Kwa nini watu wengi hawana kipato cha kutosha? Kwa nini watu wengi hawana biashara zenye mafanikio? Kwa nini?

Jibu ni hili, licha ya dunia kuwa na utele lakini unakipata unachofanyia kazi na sio unachokitamani au kukitaka. Hata kama hewa safi imejaa duniani, una jukumu la kutoa chafu na kuvuta iliyo safi. Hata kama bahari imejaa samaki, huwezi kuwakuta wamefika jikoni mwenyewe. Unahitaji kufanyaia kazi. Unapata unachofanyia kazi.

Kumbe kama kuna vitu ulitamani sana uwe navyo maishani na huna, tambua kuwa bado hujavifanyia kazi. Na njia pekee ya kuvipata ni kufanyia kazi, na hakuna njia nyingine.

Tupo mwishoni kabisa mwa mwaka 2022 tukiwa tunajiandaa kuingia mwaka 2023. Inawezekana kuna vitu ulivitamani uwe navyo mwaka huu lakini mpaka sasa hujavipata kwa sababu hujavifanyia kazi. Jipange kuhakikisha mwaka huu unavipata. Utavipataje?

Tambua kwa dhati nini unataka . Weka wazi kabisa akilini mwako nini unakitaka. Akili yako itaweza kukusaidia kukipata unachokitaka kama utiwekea wazi ni unataka. Kama ni kipato, basi weka wazi unataka kupata kipato cha sh….. mwaka 20. Unataka kuwa tajiri, hongera, utajiri wa shilingi?

Tambua gharama za kulipa. Tumeona kuwa hata kama bahari imejaa samaki ni lazima uende ukavue ndipo uwapate samaki hao. Hii ni gharama ya kupata utele huo. Kwenye kila kitu unachokitaka, kuna gharama za kulipa. Weka bayana ni vitu gani unatakiwa kuvifanya ili upate unachokitaka.

Lipa gharama hizo. Watu wengi wanafahamu nini wanachotakiwa kufanya ili waweze kupata wanachokitaka, lakini hawafanyi hivyo. Ndugu! Vitu havitokei ‘automatiki’, unahitaji utayari wa kulipa gharama hizo. Hakuna mbadala lipa gharama. Hakuna mbadala weka kazi. Hapa huhitaji kujiuliza kama unapenda kulipa au la, unahitaji kujisukuma.

Unakipata unchofanyia kazi sio unachokitaka. Umetamani kwa muda mrefu sasa, ni wakati wako wa kuweka kazi yaani kulipa gharama ili ukipate ulichokitamani kwa siku nyingi.

Kitabu cha DONDOO 366 ZA MAFANIKIO YA MAFANIKIO ni mwongozo mzuri wa kukusaidia kukipata unachokitaka kwa mwaka 2023. Kitabu hiki kinakujengea nguzo 12 za mafanikio ndani yako. Nguzi hizo ni kama, kutambua nguvu yako ya pekee, kujenga maona na melengo, kazi na nidhamu, ustahimilivu nk.

Kitabu hiki kina DONDOO 366 ambapo utasoma, kuitafakari na kuchukua hatua kwa DONDOO moja kila siku kwa mwaka mzima. Ni hakika utapata unachokifanyia kazi.

Bei ya kitabu hiki ni sh 20,000/, lakini kwa sababu natamani mwaka 2023 ukipate ulichokisubiri siku nyingi, utakipata kwa sh.15,000/. Wahi ofa hii kabla haijaisha. Mawasiliano: 0752 206 899. Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *