Je Unataka Kubadili Maisha Yako! Anzia Hapa.
Je unaridhika na maisha unayoishi sasa? Kama jibu ni hapana, ina maana hayo siyo maisha unayostahili, hivyo unahitaji kubadili maisha hayo.
Wapi kwa kuanzia kubadili maisha yako, imekuwa changamoto kwa watu kwa watu wengi. Wapo wengi waliokwamia hapo. Harvey Specter alisema “If you want to change your life change your mind” akimaanisha kuwa kama unataka kubadili maisha basi badili mtazamo wako.
Kubadili maisha yako na kupata kile unachostahili fuata hatua zifuatazo;
[ ] Amua kubadili maisha yako. Hali uliyonayo sasa kiwe kichocheo cha wewe kufanya mabadiliko. Huwezi kubadilika kama hutaamua kufanya hivyo. Ona haja ya kubadili ndipo utachukua hatua ya kubadilika. Pia hutaamua kubadilika kama hakuna kitu kinachokusukuma ubadilike. Tumia hali yoyote inayokuudhi sasa kubadilika.
[ ] Tambua mabadiliko unayotaka yatokee. Unataka nini? Matokeo gani unataka uyapate. Baada ya mabadiliko kufanyika nini unataka ukipate maishani? Hii ni sababu ya mabadiliko. Sababu hii lazima iwe wazi ili ikusukume kubadili mtazamo wako. Kumbuka kuwa sababu hiyo lazima ikubalike na ijengeke akilini mwako.
[ ] Kuwa tayari kukabiliana na ukinzani. Kubadili mtazamo ni kubadili imani. Kubadili imani ni jambo gumu sana. Hii ni kwa sababu ya imani hiyo kuzama sana ndani yako. Kufanya mabadiliko haya ni kitu ambacho kitakuwa kinakukera sana. Kuwa tayari kuvumilia hilo.
[ ] Tambua kitu kinachoweza kukukwamisha. Wakati wa mabadiliko kuna vitu vinavyoweza kukukwamisha. Kumjua adui ni nusu ya kushinda. Kama ni marafiki zako, au ratiba yako nk viainishe hivyo na njoo namna ya kuepukana navyo.
[ ] Chagua kitu kimoja kwanza. Kulingana na mabadiliko unayotaka kuyafanya, unaweza una vitu vingi unavyotakiwa kuvifanya. Usifanye vyote kwa pamoja, vinaweza kukuvunja moyo. Ili uweze kufanya mbadiliko chagua kimoja, kamilisha kisha endelea na kingine. Kama mabadiliko unayotaka kuyafanya ni kuwahi kuamaka, kuweka akiba, kuacha ulevi nk, anza na moja, anza kuwahi kuamka ukifanikiwa hilo, nenda, kuweka akiba nk
Kubadili maisha yako ni kubadili mtazamo. Je unataka mafanikio kwenye mwaka 2023? Anza kwa kubadili mitazamo.
Kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO kinaelezea nguzo 12 zinazojenga mafanikio yako ya kudumu maishani mwako. Nguzu mojawapo ni mtazamo sahihi. Nakushauri ukipate kitabu ili kiwe ufunguo muhimu sana mafanikio yako ya mafanikio mwaka 2023.
Jipatie kitabu hiki kwa bei ya promotion ya mwaka mpya. Lipia sh 15,000/ badala ya sh 20,000/. Wahi ofa hii leo. Mawasiliano: 0752 207 899.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz