SEMINA! SEMINA! SEMINA!     PANGA KISHA TIMIZA  


Categories :


 
MAADA: KUJENGA NIDHAMU KALI YA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO YAKO

Je umekuwa ukiweka malengo kila mwaka lakini mwaka huo unaisha ukiwa huna matokeo? Inatosha sasa!  Pata picha umeweka malengo mazuri ya mwaka 2023 kisha ukafanikiwa kuyafanyia kazi na yakakupatia matokeo makubwa ambayo hujawahi kuyapata. Utajisikiaje? AMSHA UWEZO imekuandalia semina inayohusu ‘’KUJENGA NIDHAMU KALI KUKUWEZESHA YA KUTIMIZA MALENGO YAKO’’ ili kuufanya mwaka 2023 wa toafuti kwako.
 
Hata kama utakuwa na malengo na mipango mizuri kiasi gani, kama unakosa nidhamu ya kukuwezesha kuchukua hatua itakuwa ni bure kabisa. Umekuwa ukiweka malengo kila mwaka lakini, changamoto yako imekuwa kutoyafanyia kazi malengo hayo kisha kupata matokeo.  Ufunguo wa mafanikio ya malengo yako ni nidhamu kali. Kupitia semina hii utajenga tabia ya kuchukua hatua uliyoyapanga hata kama hujisikii au mambo yanapokuwa magumu.
 
 Zaidi ya nidhamu ya kukuwezesha kufanyia kazi malengo yako ya mwaka 2023 pia utachagua lengo/jambo moja  ambalo utahamasishwa kulifanya kila siku kwa mwaka mzima bila kuacha. Pata picha ukaamua kuandika maneno 100 tu kila siku, mwaka utakapoisha utakuwa na meneno 36,000 ambayo yanaweza kuwa kitabu kilichokamilika. Pata picha tena ukaamua kuweka akiba ya sh 1,000/ tu kila siku, mwaka utakapoisha utakuwa na sh 365,000/. Hii ni fedha ambayo unaweza kuitumia kama mtaji na ikazalisha zaidi.
 
MAADA: KUJENGA NIDHAMU KALI YA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO YAKO
 
1. NIDHAMU NA MAFANIKO

Maana ya nidhamu

Aina za nidhamu

Nidhamu na mafanikio

 
2. NIDHAMU NA MELENGO

Maana ya Malengo

Sifa za malengo

Vipande vya malengo

Nidhamu na malengo

 
3. KUJENGA NIDHAMU

Msingi wa kujenga nidhamu

Nidhamu kama tabia

Hatua za kujenga nidhamu

 
4. NIDHAMU BINAFSI

Maana ya nidhamu binafsi

Nidhamu binafsi unazopaswa kuzijenga

Namna ya kujenga nidhamu binafsi

 
5. NIDHAMU YA MUDA

Muda na mafanikio

Jitenge naa kelele za dunia

Kukabiliana na ugonjwa wa kuahirisha

Kuwa na uzalishaji mkubwa

 
6. NIDHAMU YA FEDHA

Chuma ulete wa fedha zako

Usifukie shimo kwa kuchimba shimi

Namna ya kujenga nidhamu ya fedha

 
7. NIDHAMU YA KAZI

Rafiki mwaminifu wa kuwa naye

Hakuna mbadala wa kazi

Namna ya kujenga nidhamu ya kazi

 
8. NIDHAMU MOJA YA KUJENGA MWAKA 2023.
·       Mifano  10 ya nidhamu unazoweza kujenga
·       Chagua angalau nidhamu moja ya kujenga 2023
 
9. MIFANO YA NIDHAMU KUTOKA KWA WATU WALIOFANIKIWA

Mafanikio makubwa na nidhamu kali ya kujirudia

Mifano ya nidhamu kutoka kwa watu waliofanikiwa

 
10. CHURA WA KUMLA KILA SIKU

Siku na mafanikio

Tathmini ya siku

Chagua chura wa siku

 
Semina hii itafanyika kwa siku kumi kwa njia ya mtandao (Kundi maalumu la Wasap) kuanzia Tarehe 18 – 27 Januari, 2023. Kila  siku utajifunza somo moja, ambapo kila siku asubuhi litawekwa somo la siku husika kwenye kundi la wasp na kupata muda wa kulisoma na kuchukua hatua unazopaswa kuchukua na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku tutapata muda wa kujadiliana na kuuliza maswali.
 
Gharama ya kushiriki semina hii ni Tsh. 10,000 (Elfu kumi tu) kwa siku zote kumi. Hii ni sawa na bure ukilinganisha na thamani ya masomo unayoenda kuipata. Lakini kwa sababu nakujali wewe ndugu yangu, nimeweka kiasi hiki ili usiikose fursa hii. Jambo ninalokuomba leo ili usiikose fursa hii ni kujiunga kwanza na kundi hili kabla nafasi hazijaa. Kujiunga bonyeza kiunganishi hiki na utajiunga moja kwa moja,  https://chat.whatsapp.com/GiQlBQKR17vI2XsSXkj7TN
Lipia malipo ya semina hii kupitia MPESA 0752 206 899 (Alfred Mwanyika). Karibu sana
 
Imeandaliwa na Alfred Mwanyika ,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio)
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz   
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *