Njia Pekee Ya Kukutana Na Unachokitaka Mwaka 2023


Categories :



Heri ya mwaka mpya. Naamini una shauku kubwa ya kupata kitu cha utofauti mwaka huu 2023. Hii ni shauku iliyokujia baada ya kuuanza mwaka mpya.

Au ni shauku iliyokuja baada ya mwaka jana kukosa kile ulichokitaka na hivyo kuona mwaka huu ni fursa nyingine ya kukipata kitu hicho. Au ni shauku iliyokua baada ya mwakajana kukupata matokeo madogo tofauti na matarajio yako.

Leo nakupa njia ya uhakika ya kukutana na kitu ulichokitafuta siku nyingi. Pata picha umekipata kitu ambacho umekuwa unakitamani siku nyingi….utajisikiaje? Naamini utajisikia vizuri sana. Njia hiyo ya kupata unachokitaka ni kutengeneza njia ya kukutana na kitu hicho.

Huwezi kufika eneo ulilolipanga kama hujajua njia ya kupitia. Sehemu unayotaka kufika ni lengo lako na njia za kukufikisha huko ni mipango.

Lakini jambo la kwanza kabla ya kutengeneza njia ni kuhakikisha unafahamu kwa wazi kabisa wapi unataka kufika. Lengo lako liwe wazi kabisa. Usiseme mwaka huu nataka kufanya makubwa, yapi hayo? Nataka kuongeza kipato, sh? Kwa hiyo kama unataka kuongeza kipato, weka wazi kabisa, nataka kuongeza kipato changu kutoka sh…….mpaka sh……… Kwa mfano nataka kuongeza kupato kutoka sh milioni 1 mpaka milioni 2 ifikapo Disemba 31, 2023.

Hivyo kwenye mfano wa hapo juu, milioni mbili ndiyo sehemu unakotaka kufika. Kujua nini unataka ni hatua ya awali tena rahisi, lakini namna ya kufika huko ndiyo changamoto kubwa kwa watu wengi. Hivyo baada ya hapo huna budi sasa kutengeneza njia za kukufikisha kwenye milioni 2.

Kutengeneza njia sahihi za kuwafikisha kwenye lengo imekuwa changamoto kwa watu wengi. Baada ya kuweka lengo, wengi huendelea kugusa vitu vingi bila mpangilio na hivyo kutotimiza melengo yao.

Kwenye mfano wa lengo la kuongeza kipato kutoka sh milioni 1 mpaka milioni 2. Hii ingeweza kuwa mipango(njia za kukufikisha);
[ ] Kuongeza uelewa wa kazi au biashara unayoifanya. Kazi au biashara haiwezi kukua kama wewe hujakua ndani yako.
[ ] Kuongeza mauzo kwenye biashara yako kwa kuwafikia wateja wengi zaidi, kuwashawishi waliopo kununua zaidi nk
[ ] Kuongeza umakini na muda wa kufanya kazi
[ ] Kama mwajiriwa, kuongeza thamani zaidi ya kazi yako na hivyo kuongezewa mshahara. Au kuanzisha biashara pembeni mwa ajira
[ ] Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
[ ] Kufungua tawi jipya la biashara yako au kuongeza huduma eneo lako la sasa la biashara.
Unaona, kumbe kuna kitu kikubwa cha kufanya baada ya kuweka lengo lako. Hizo ndizo za kukufikisha unakotaka kwenda.

Lakini ili uweze kupita kwenye njia hizi na kutimiza malengo yako kuna usafiri mmoja muhimu sana inabidi uupande. Na bila usafiri huo, utaishia njiani. Kwa sababu wengi wamekuwa hawaupandi, idadi kubwa ya watu pia wameshindwa kutimiza malengo yao. Wewe mwaka huu upande kwenye usafiri huo unaoitwa NIDHAMU.

Nidhamu ni kufanya kile ulichokipanga bila kusikiliza sababu yoyote. Hiki ndicho kimekuwa kinakukwamisha kila mwaka.

Ili kuhakikisha mwaka huu hukwami, AMSHA UWEZO imekuandalia semina ya siku kumi inayohusu KUJENGA NIDHAMU KALI YA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO YAKO. Semina itahakikisha unakaa kwenye njia kufikia melengo yako.

Zaidi ya nidhamu ya kukuwezesha kufanyia kazi malengo yako ya mwaka 2023 pia kwa kushiriki utachagua lengo/jambo moja  ambalo utahamasishwa kulifanya kila siku kwa mwaka mzima bila kuacha.
[ ] Je ni kuamka mapema na kuianza siku kwa ushindi?
[ ] Je ni kusoma kila siku kisha kufanikiwa kumaliza kitabu kikubwa kila mwezi na hivyo vitabu 12 na kuona suluu nyingi za matatizo yako.
[ ] Je ni kuweka akiba hata ya sh 1000 kila siku kwa mwaka mzima?
[ ] Je nikufanya mazoezi kila siku na kuiamarish afya?
Utakuwa na chaguo moja kati ya mengi yatakayokuwepo.

Semina hii itafanyika kwa siku kumi kwa njia ya mtandao (Kundi maalumu la Wasap) kuanzia Tarehe 18 – 27 Januari, 2023.

Gharama ya kushiriki semina hii ni Tsh. 10,000(Elfu kumi tu) kwa siku zote kumi. Jambo ninalokuomba leo ili usiikose fursa hii ni kujiunga kwanza na kundi hili kabla nafasi hazijaa. Kujiunga bonyeza kiunganishi hiki na utajiunga moja kwa moja
https://chat.whatsapp.com/GiQlBQKR17vI2XsSXkj7TN

Lipia malipo ya semina hii kupitia MPESA 0752 206 899 (Alfred Mwanyika). Karibu sana.

Mwl. Alfred Mwanyika
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *