Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa ‘Jiniasi’ Mwaka Huu 2023.
Huyu ni ‘Jiniasi’ haya ni maneno ambayo amekuwa akiambiwa mtu ambaye anafanya kitu fulani kwa uwezo mkubwa na kisha kupata matokeo makubwa na ya kushangaza. Majiniasi wameonekana kuwa watu wa pekee sana na wamependelewa.
Lakini ni kweli Majiniasi ni watu waliopendelewa? Je wewe siyo Jiniasi? Je huwezi kuwa Jiniasi sasa?
Maswali ya majibu hayo yalijibiwa na mwanasayansi nguli Albeet Einstein kwenye nukuu hii : “Genius is 1% talent and 99% percent hard work…” ikitafsiriwa kuwa Ujiniasi ni 1% tu kipaji na 99 bidii.
Kumbe kuna kazi kubwa ya kufanya baada ya kuzaliwa ili uweze kuonyesha ujiniasi wako. Matokeo makubwa yatakayowashangaza watu yanahitaji kazi kubwa sana kutoka kwako.
Ubunifu utakaoufanya na ukawashangaza watu na baadaye kuwa tayari kulipia kazi hiyo inahitaji kazi na bidii kubwa.
Thamani kubwa utakayokuwa unaitoa kwa watu na watu wakawa tayari kulipia gharama hiyo kubwa haitakuja yenyewe bali kwa bidii na kazi kubwa utakayofanya.
Ndugu, una nafasi kubwa ya kufanya makubwa katika maisha yako. Kuna kitu cha kipekee ambacho hata moyo wako huwa unakushuhudia ukifanye, huko ndiko ujiniasi wako uliko.
Lakini ujiniasi huo hautaonekana bila kuweka bidii na kazi kubwa. Albert ameonyesha wazi kuwa ili uweze kuwa jiniasi, kuna 99% za kuweka kazi tena kubwa.
Hata wewe unauwezo wa kuonyesha matokeo ya kipekee mwaka huu 2023. Matokeo ambayo kila mtu atakushangaa na kuona wewe si mtu wa kawaida. Unaweza kuweka malengo makubwa sana na kisha kupata matokeo makubwa sana.
Lakini kazi hiyo itaweza kufanyika kama utapata kiungo hiki muhimu cha matokeo; nacho ni nidhamu.
NIDHAMU ni kuweza kufanya kile ulichopanga bila kuruhusu sababu yoyote ile ikuzuie. Tabia hii ndiyo inayowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Wanaofanikiwa ni wale wanojenga nidhamu kali ya kufanya kile kinachotakiwa kufanywa ili kuweza kupata matokeo bila kuruhusu sababu yoyote. Wanaoshindwa, baada ya kuweka mipango, wanafanya tu kazi pale wanapojisikia na wanaruhusu sababu ziwazuie kuchukua hatua.
Ndugu! Mwaka huu 2023 panga kuwa Jiniasi kwa kuhakikisha unaweka bidii na kazi kubwa kwenye malengo yako.
Kufanikisha hilo, kampuni ya AMSHA UWEZO imekuandalia semina ya siku kumi kuhusu KUJENGA NIDHAMU KALI YA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO. Hii ni semina ya kukufanya upate matokeo makubwa ya ajabu kutoka kwenye malengo yako.
Pata picha Disemba imefika na umefanikiwa kupata matokeo makubwa ambayo hujawahi kuyapata maishani mwako! Utajisikiaje?
Zaidi ya nidhamu ya kukuwezesha kufanyia kazi malengo yako ya mwaka 2023 pia kwa kushiriki utachagua lengo/jambo moja ambalo utahamasishwa kulifanya kila siku kwa mwaka mzima bila kuacha.
[ ] Je ni kuamka mapema na kuianza siku kwa ushindi?
[ ] Je ni kusoma kila siku kisha kufanikiwa kumaliza kitabu kikubwa kila mwezi na hivyo vitabu 12 na kuona suluu nyingi za matatizo yako.
[ ] Je ni kuweka akiba hata ya sh 1000 kila siku kwa mwaka mzima?
[ ] Je nikufanya mazoezi kila siku na kuiamarisha afya?
[ ] Je ni kuongezeka mteja mmoja tu wa biashara yako kisha kukuza mauzo mara dufu?
Utakuwa na chaguo moja kati ya mengi yatakayokuwepo.
Semina hii itafanyika kwa siku kumi kwa njia ya mtandao (Kundi maalumu la Wasap) kuanzia Tarehe 18 – 27 Januari, 2023.
Gharama ya kushiriki semina hii ni Tsh. 10,000(Elfu kumi tu) kwa siku zote kumi. Jambo ninalokuomba leo ili usiikose fursa hii, ni kujiunga kwanza na kundi hili kabla nafasi hazijaa. Kujiunga bonyeza kiunganishi hiki na utajiunga moja kwa moja kwenye kundi hilo maalumu la semina.
https://chat.whatsapp.com/GiQlBQKR17vI2XsSXkj7TN
Lipia malipo ya semina hii kupitia MPESA 0752 206 899 (Alfred Mwanyika). Karibu sana.
Mwl. Alfred Mwanyika
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899