Usihangaike Tena, Huyu Ndiye Aliyebeba Hatima Yako.
Ndugu yangu! Kumbuka tena leo kitu ambacho umekuwa ukikitamani kukipata kwa muda mrefu lakini bado hujakipata.
Umekuwa ukiumiza kichwa ni kwa namna gani unaweza utafanikiwa kukipata kitu hicho.
Kuna muda umefikiria kuwa wazazi wako ndiyo wanajukumu la kuamua hatima ya maisha yako. Kuna wakati umefikiri kuwa serikali yako ndiyo inayowajibika kukupa ukitakacho.
Ndugu! Utawaonea watu wengu bure! Yupo mtu mmoja anayeweza kuamua hatima ya kile unachokitaka, naye ni wewe mwenyewe.
Ndiyo, hakuna mtu mwingine atakayekupa unachokitaka isipokuwa wewe.
Wewe ndiye mhusika mkuu wa kile unachokitaka. Na nakuhakikishia kuwa unaweza kupata kile unachokitaka.
Je unataka utajiri? Je unataka afya njema? Je unataka kuwa mtu wa thamani kwa watu wengine? Je unataka ridhiko la moyo? Je unataka umaarufu?
Unaweza kupata chochote hapo na vingine lakini baada ya kutambua kuwa wewe ndiye muhusika mkuu.
Kuna kitu kimoja unachotakiwa kufanya baada ya kuchukua jukumu la kukipata unachokitaka, nalo ni kujenga nidhamu kali.
Nidhamu kali ni ufunguo wa kukuwezesha kupata chochote. Nidhamu kali ni tabia ya kufanya kilichosahihi ili kupata matokeo bila kukubali kitu chochote kikuzuie.
Kujenga nidhamu hii kunakuhitaji kujitoa hasa. Wengi wameshindwa lakini inawezekana. Waliofanikiwa wameweza kujenga tabia hii muhimu.
Ndugu! Amaua mwaka huu kuwa wa maajabu kwako. Jenga nidhamu kali itakayokufanya upate matokeo ambayo yatakupa unachotaka.
AMSHA UWEZO Imekuandalia semina inayohusu KUJENGA NIDHAMU KALI YA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO YAKO.
Semina hii inakusaidia kujenga nidhamu kali itakayokuwezesha kupata ufunguo(NIDHAMU KALI) wa kukuwezesha kupata chochote maishani mwako.
Nidhamu za kujenga utakazojifunza ni nidhamu binafsi, muda, kazi, fedha nk.
Zaidi ya nidhamu ya kukuwezesha kutimiza malengo yako ya mwaka 2023 pia kwa kushiriki utachagua lengo/jambo moja ambalo utahamasishwa kulifanya kila siku kwa mwaka mzima bila kuacha.
[ ] Je ni kuamka mapema na kuianza siku kwa ushindi?
[ ] Je ni kusoma kila siku kisha kufanikiwa kumaliza kitabu kikubwa kila mwezi na hivyo vitabu 12 na kuona suluu nyingi za matatizo yako.
[ ] Je ni kuweka akiba hata ya sh 1000 kila siku kwa mwaka mzima?
[ ] Je nikufanya mazoezi kila siku na kuiamarisha afya?
[ ] Je ni kuongezeka mteja mmoja tu wa biashara yako kisha kukuza mauzo mara dufu?
Utakuwa na chaguo moja kati ya mengi yatakayokuwepo.
Semina hii itafanyika kwa siku kumi kwa njia ya mtandao (Kundi maalumu la Wasap) kuanzia Tarehe 18 – 27 Januari, 2023.
Gharama ya kushiriki semina hii ni Tsh. 10,000(Elfu kumi tu) kwa siku zote kumi. Jambo ninalokuomba leo ili usiikose fursa hii, ni kujiunga kwanza na kundi hili kabla nafasi hazijaa. Kujiunga bonyeza kiunganishi hiki na utajiunga moja kwa moja kwenye kundi hilo maalumu la semina.
https://chat.whatsapp.com/GiQlBQKR17vI2XsSXkj7TN
Lipia malipo ya semina hii kupitia MPESA 0752 206 899 (Alfred Mwanyika). Karibu sana.
Mwl. Alfred Mwanyika
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899