Huwezi Ukampuuzia Huyu, Halafu Ukabaki Salama.
Moja ya mbinu ambayo watu hutumia kuachana na kitu ambacho hakina thamani kwao ni kupuuzia. Mtu anaweza kumpuuzia mtu mwingine ili asimpotezee umakini au muda.
Unapofikia hatua ya kupuuzia, ina maana umekuwa tayari kukipoteza kitu hicho.
Lakini sasa watu wameenda mbali zaidi wakipuzia kitu ambacho ndiyo kimeshikiria mafanikio yao. Kitu hicho ni muda.
Imekuwa rahisi mtu kuuacha muda upotee tu bila kufanya kitu cha maana. Wengine wamefiriki kusema ngoja aende sehemu fulani akapoteze muda.
Ndugu huu ni upuuziaji wa kiwango cha juu sana. Huwezi ukaupuzia muda, halafu ukabaki salama, lazima ikugharimu.
Maisha yako ni muda. Mafanikio yako ni muda. Wewe ni muda. Bila muda hakuna chochote. Ndiyo maana kuna kauli hii maarufu inayosema muda ni mali, au muda ni fedha.
Hivyo huwezi kuwa na mali kama utaupuuzia muda. Huwezi kuwa tajiri kama utaupuuzia muda. Huwezi kufikia ukuu wako kama hutauheshimu muda wako.
Yaani muda ndiyo maisha yako. Muda wako wa kuishi hapa duniani ukiisha hakuna kitu kingine unachoweza kukifanya.
Njia pekee ya kuuheshimu muda na wenyewe ukakuheshimu ni kuwa na nidhamu ya muda. Tena sio nidhamu tu ya kawaida, bali nidhamu kali.
Hii ni tabia ya kufanya kitu sahihi kwenye muda ulioupanga bila kusikiliza vikwazo vyovyote vile vinavyoweza kujitokeza.
Kujenga nidhamu kali ya muda imekuwa changamoto kwa watu wengi, ndiyo maana ni wachache sana wamefanikiwa kuwa nayo. Hao ndiyo waliopata mafaniko ya hali ya juu.
Ndugu yangu, na wewe ukifanikiwa kujenga nidhamu hii ya muda utapata heshima ya mafanikio. Kwa sababu bado upo hai, sahau upuuziaji uliofanya, jisukume kuuheshimu sasa.
AMSHA UWEZO Imekuandalia semina inayohusu KUJENGA NIDHAMU KALI YA KUKUWEZESHA KUTIMIZA MALENGO YAKO.
Semina hii inakusaidia kujenga nidhamu kali itakayokuwezesha kuupa muda heshima yake na kisha nao ukakupatia chochote unachokitaka.
Zaidi nidhamu ya muda nidhamu nyingine utakazojifunza ni nidhamu binafsi, ya kazi, fedha nk.
Si hivyo tu, zaidi ya kuweza kujenga nidhamu ya kutimiza malengo yako ya mwaka 2023, utapata fursa ya kuchagua jambo moja ambalo utalifanya kila siku kwa mwaka mzima bila kuacha;
[ ] Je ni kuamka mapema na kuianza siku kwa ushindi?
[ ] Je ni kusoma kila siku kisha kufanikiwa kumaliza kitabu kikubwa kila mwezi na hivyo vitabu 12 na kuona suluu nyingi za matatizo yako.
[ ] Je ni kuweka akiba hata ya sh 1000 kila siku kwa mwaka mzima?
[ ] Je nikufanya mazoezi kila siku na kuiamarisha afya?
[ ] Je ni kuongezeka mteja mmoja tu wa biashara yako kisha kukuza mauzo mara dufu?
Semina hii itafanyika kwa siku kumi kwa njia ya mtandao (Kundi maalumu la Wasap) kuanzia Tarehe 18 – 27 Januari, 2023.
Gharama ya kushiriki semina hii ni Tsh. 10,000(Elfu kumi tu) kwa siku zote kumi. Jambo ninalokuomba leo ili usiikose fursa hii, ni kujiunga kwanza na kundi hili kabla nafasi hazijaa. Kujiunga bonyeza kiunganishi hiki na utajiunga moja kwa moja kwenye kundi hilo maalumu la semina.
https://chat.whatsapp.com/GiQlBQKR17vI2XsSXkj7TN
Lipia malipo ya semina hii kupitia MPESA 0752 206 899 (Alfred Mwanyika). Karibu sana.
Mwl. Alfred Mwanyika
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899