Hili Ndilo Eneo Lako La Kujidai.
Ukimuona nyani akiwa msitini akiruka kutoka tawi moja la mti kwenda jingine utadhani yeye ndiye aliye umba matawi hayo na kuwa ana gundi miguuni mwake. Hili ni eneo lake la kujidai.
Ukimuona samaki akiwa majini akiogelea kwa maringo utasema anaijua kweli sayansi ya maji. Maji ni eneo lake la kujidai. Lakini ukimtoa nje ya maji anakufa.
Ukiiona ndege ikiwa na uzito mkubwa ikielea hewani bila kuanguka usishangae kwa sababu ipo kwenye eneo lake la kujidai. Lakini ikiwa majini haiwezi kufanya chochote.
Nataka nikukumbushe kitu kimoja leo kuwa hata wewe una eneo lako la kujidai. Ukiwa kwenye eneo hilo ndipo watu wanapoweza kukushangaa.
Kama sahizi upo sehemu na hakuna mtu anayekushangaa kwenye yale unayoyafanya, basi tambua ni ama hupo kwenye eneo lako la kujidai au upo huko lakini hujaanza kuishi eneo hilo.
Eneo la kujidai ni upekee wako. Ni kitu ambacho unaweza kukifanya kwa uwezo wa hali ya juu sana kiasi kwamba matokeo yake yakawashangaza wengi.
Wengine wanaweza kujaribu kitu hicho unachokifanya lakini watafanya kwa ugumu na matokeo hayatakuwa makubwa kama yako.
Eneo lako la kujidai linahusisha kutambua na kutumia kipaji chako. Hii ni nguvu ya pekee uliyonayo.
Utayapata mafaniko makubwa kama utaunganisha kipaji chako na mipango ya kutoa thamani kwa watu wengine.
[ ] Kama kipaji chako ni kuimba basi anzisha na kukuza biashara inayohusisha kuimba. Ndipo utakapoweza kustahimili changamoto zote na kutoa thamani kubwa kwa watu wengine na wakawa tayari kukulipa
[ ] Kama kipaji cha ni uandishi basi anzisha na kukuza biashara itakayolenga kutoa maarifa yenye thamani kubwa sana kwenye eneo ulilolichagua
[ ] Kama kipaji chako ni ualimu basi wekeza kwenye kutoa mafunzo ambayo hayatakuwa rahisi kupatikana sehemu nyingine yoyote
Kipaji chako ni kipi? Eneo lako la kujidai ni lipi. Unatoa nini cha thamani ili dunia ikufuate. Licha ya nyuki kwenda mbali sana kisha kutengeneza asali, lakini bado binadamu humfuata huko. Si kwa sababu wanataka kukutana na nyuki la hasha! Bali asali anayoitengeneza.
Kwa sababu ya thamani kubwa anayoitoa kwenye asali basi dunia nzima inamtambua nyuki.
[ ] Je unahitaji umaarufu? Kaka kwenye eneo lako la kujidai
[ ] Je unataka utajiri? Kaa kwenye eneo lako la kujidai
[ ] Je unataka kukua na kufikia ukubwa wako? Basi kaa kwenye eneo lako la kujidai
[ ] Unataka kuridhika maishani? Basi kaa kwenye eneo lako la kujidai
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kimeelezea kiundani kuhusu upekee wako na kipaji chako. Kitabu kinakupa mwongozo wa kutambua nguvu kubwa iliyolala ndani yako na namna ya kuiamsha ili uweze kufanya makubwa.
Kitabu hiki kitakuongoza kutambua kipaji chako na kukitumia kukaa kwenye eneo lako la kujidai.
Bei ya kitabu hiki ni sh 15,000/. Lakini kwa leo utakipata kwa bei ya ofa ya sh. 10,000/. Lengo ni kuhakikisha wewe unakipata kitabu hiki ili kiweze kukupeleke eneo lako ka kujidai.
Utajisikiaje kama utafanikiwa kutambua na kisha kukaa kwenye eneo lako la kujidai ukiwa na mafanikio makubwa na ridhiko la moyo wako?
Basi amua sasa kukipata kitabu hiki. Wasiliana nami kupitia 0752 206 899.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Halisi na Mafanikio)
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz