Hiki Ni Kizuri Zaidi Kuliko Ulichoamua Kufanya .


Categories :

Itakuwaje kama nitafanya halafu nikashindwa? Watu watanichuliaje kama nikianzisha kitu halafu nikashindwa? Watu watanionaje kama nikiisema na kuanza kuiishi hii ndoto yangu kubwa, si wataniona chizi? Itakuwaje kama nikianzisha biashara halafu ikafa, si nitakuwa nimepoteza fedha zangu?

Haya ni maswali uliyojiuliza na kwa sababu majibu yale yalikuwa hayakupatii uhakika wa matokeo chanya moja kwa moja, basi ukaamua kutokuanza.

Lakini kuna maamuzi ambayo yalikuwa mazuri zaidi kuliko uliyoyafanya. Nayo ni kuanza kile
ulichoogopa kuanzisha.

Ukianza utatoa ukinzani

Kuanza ndiyo kunakupa nafasi ya kuendelea na kukua. Huwezi ukaendelea na safari unayotaka kusafiri kama hutatoa hatua ya kwanza. Safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja. Unataka makubwa, anza hata kwa kidogo.

Kuanza kunakupa nafasi ya kujua ulichonacho na ulichopungukiwa. Ukianza utajua kama ulichokuwa unafikiri unakijua au la. Huwezi kujua uimara au udhaifu wako mpaka uanze kufanya. Hivyo anza.

Kuanza hukupatia uhalisia wa mambo. Mipango unayoiweka ni nadharia lakini kuna uhalisia wakati wa kufanya. Wanasema mipango si matumizi. Si kila unachopanga kinatokea kama ulivyotarajia. Hivyo anza uone unapata nini kwenye ulichopanga?

Kuanza kimekuwa ni kitu kigumu sana kwa watu wengi. Kwa sababu kuanza;
Kuanza huogofywa kwa sababu ya majibu huna uhakika wa majibu.
Kuanza huhitaji nguvu kubwa, muda mwingi, umakini mkubwa; ndiyo maana watu husita

Kwa sababu ya mchakato mgumu wa kuanza, ndiyo maana umekuwa ukichukua uamuzi huo mwingine wa kuahirisha kuanza.

Ndugu, hakuna matokeo utakayopata kwa kuamua kuahirisha au kuacha kuanza. Kila kitu unachotaka ukipate, huwa kinakuwa mwanzo. Mwanzo huwa haufurahishi lakini kutokuanza ni kupotea kabisa.

Kaa chini na tafakari ni vitu gani ulitakiwa uvianzishe lakini hukufanya hivyo. Kumbuka

[ ] Kama ungekuwa umeianzisha biashara sahizi ingekuwa ilishakuwa na kukupa faida kubwa

[ ] Kumbuka ungekuwa umeanza kuandika kitabu kingekuwa kimeshaisha na ndoto yako imetimia

[ ] Kama ungekuwa umeanza kusoma kitabu, cha kwanza kingekuwa kimeisha na umehamia kingine

[ ] Kama ungekuwa umeanza kuweka akiba, sahizi ungekuwa na kiasi kikubwa hata cha kutosha kuanzisha biashara

[ ] Kama ungekuwa umeanza kujenga tabia hata ya kauamka mapema, sahizi ungekuwa tayari umeshazoea na siku zako kuwa na ufanisi mkubwa.

Kitu gani utaanza kukifanya leo?

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Halisi na Mafanikio)
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *