*Usipige Mbizi Sakafuni, Utaumia!*


Categories :

Ukimuona mtu kama anaogelea sakafuni ambako hakuna maji yoyote utamshangaa sana. Ni rahisi sana kumfikiria kuwa atakuwa amechanganyikiwa.

Imezoeleka kuwa watu huogelea majini, ndiyo maana itakuwa ni ajabu sana kumkuta mtu anaonekana kuogelea angali hayupo kwenye maji.

Lakini nasikitika kukuambia kuwa hiki ni kitu ambacho umekuwa ukikifanya maishani mwako. Kuogelea si jambo la kushangaza, lakini kuogelea sakafuni ndiyo ajabau. Kuogelea sakafuni kutakupa maumivu kwa sababu si sehemu sahihi au namna sahihi.

Kuogelea sakafuni ni kuishi maisha kwa namna ambayo husitahili kuishi kwa namna hiyo. Huku ni kuishi kwa namna ambayo inaweza kukuumiza. Umeumizwa mara nyingi kwa sababu ya kujaribu kuogelea sakafuni.

*Kufanya mambo yasiyo na tija.* Unaishi kwa sababu ya muda. Kupewa muda wa kuishi ni usahahi, lakini kutumia muda huo kufanya mambo yasiyochangia kwenye kufikia ukuu wako ni kuamua kupiga mbizi sakafuni. Kutumia muda wako kupiga majungu, kuzurura kwenye mitandao ya jamii. Huku ni kupiga mbizi sakafuni na muda na kutaka kuumia.

*Kuishi bila malengo wala mipango.* Malengo ndiyo dira ya maisha yako. Malengo hukuonyesha wapi uende na kwa nini uende huko. Kuishi bila malengo ni kuamua kwenda kokote na ni rahisi kupotea na kugonga jiwe. Huku ni kuamua kuogelea sakafuni na kupotea mahali sahihi kwa kuweka nguvu, muda na umakini wako.

*Kuamini huhitaji maarifa.* Ni kweli umekuwa ukisoma na una ufaulu mzuri darasani. Lakini hii ni elimu ya darasani unahitaji elimu zaidi ya maisha. Kuna mafanikio umeyapata. Ni sawa, lakini ili upige hatua kubwa zaidi unahitaji maarifa zaidi. Kujiaminisha kuishi bila kujiendeleza binafsi kupitia maarifa ni kuamua kupiga mbizi sakafuni. Lazima utaumia tu.

*Kuishi bila kutambua upekee/kipaji chako.* Usipojua kuwa ni nyoka ndiyo anayeweza kuogelea sakafuni, ni rahisi sana na wewe kulala na kumuiga anachokifanya nyoka. Lazima ukutane na maumivu. Usiwe mtu wa kuiga wanachokifanya watu wengine bali tambua wewe ni wa pekee na kwenye upekee huo ndiko kwenye ukuu wako.

Samaki ni fundi wa kuogelea lakini majini. Siku atakayosema anaweza kuogelea sehemu yoyote hata kwenye mchanga, anakuwa amechagua kujiumiza na kifo kabisa.

[ ] Ndugu! Una namna sahihi ya kutumia maisha yako nayo ni kuishi kusudi lako.

[ ] Una namna sahihi ya kutumia muda wako, nayo ni kwenye mambo yanayochangia mafanikio yako makubwa.

[ ] Kuna namna sahihi ya kuendesha maisha yako, nayo ni kuweka malengo na mipango kisha kuifuata.
Kuna namna sahihi ya kujali maisha yako nayo ni kuwa wewe halisi.

Acha leo kuogelea sakafuni kwa kufanya kikicho sahihi katika maisha yako muda wote.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *