Nguzo Za Mafanikio Ya Maisha Yako.


Categories :

Linapokuja swala la kujenga mafanikio, ni sawa tu na kujenga ghorofa. Ghorofa huhitaji msingi imara na wa kudumu.

Ghorofa huimarishwa na nguzo ambazo husimikwa maeneo tofauti ili nyumba hiyo kuwa imara. Kujenga nyumba kubwa kama ghorofa bila kuweka nguzo ni sawa na kujidanganya kwani ghorofa hilo huweza kuondoka hata kabla ya halijamalizika kujengwa.

Mafanikio ya maisha yako pia yanahitaji nguzo ambazo ndizo zinatashikilia jitihada unazoziweka kila siku ili zikupe matokeo unayostahili.

Tumeshuhudia watu wakiwa bise na kuchoka kila siku. Lakini ni wachache sana ambao mafanikio wanayoyapata yanaendana na ubise walionao. Kadhalika, wapo wanaopata mafanikio lakini mafanikio hayo hayadumu, yaani yanaporomoka muda mfupi tu baada ya kuyapata. Changamoto ni kuwa hakuna nguzo za kushikilia mafanikio hayo.

Ndugu ni muda gani umepita tangu ulipotamani kuwa na maisha ya mafanikio ya kudumu? Jitihada ulizoziweka kwa muda mrefu zimekupa mafanikio gani? Mafanikio yako hayakui au kudumu kwa sababu yamekosa nguzo za kuyashikilia.

Leo nitakushirikisha nguzo mbili kati ya 12 zilizoelezwa kiundani kwenywe kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Nguzo ya kwanza: KUSUDI NA UWEZO. Hii ni nguzo ya kwanza kabisa kuielewa na kujienga ili uweze kuwa na mafanikio makubwa unayostahili. Kusudi ni sababu ya kitu fulani kuwepo. Kila binadamu ana sababu ya kuwepo hapa duniani. Hata wewe unayesoma hapa una kusudi lako hapa duniani bila kujali unalijua au la.

Maisha yako yatakuwa ya mafanikio makubwa kama utatambua kusudi lako na kuliishi. Ni mwanya gani unauona na unaona unaweza au wajibika kuuziba? Ni tatizo gani unaona unasukumwa kulitatua? Huu unaweza kuwa mwanzo wa kujua kusudi lako.

Uwezo ni nguvu iliyoalala ndani yako ambayo bado haijatumika. Hii ni nguvu inayokusubiri uiamshe ili uweze kufanya miujiza katika dunia hii. Hii ni nguvu ya kukuwezesha kuliiishi kusudi lako, kuitimiza ndoto yako na kuwa wewe halisi.

Nguzo ya pili: UPEKEE. Licha ya dunia kuwa na watu zaidi ya bilioni 8 na Tanzania kuwa na watu zaidi milioni 60 bado kuna WEWE mmoja tu hapa duniani. Hii ni ishara kuwa kuna kitu cha pekee kipo ndani yako ambacho hakiwezi kupatikana kwa mtu mwingine.

Kuna uwezo wa pekee ndani yako unaoweza kuipa dunia thamani ya pekee. Hii ndiyo siri ya utajiri wako. Ukitambua vipaji na karama zakona kuziishi, mafanikio ni lazima.

Ndugu, hay ni maelezo mafupi tu ya nguzo mbili kati ya 12 zilizopo kwenye kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Naamini upo kama mimi unayependa kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako. Kulitimiza hilo hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki leo.

Habari njema ni kuwa kitabu hiki kinapatikana kwa vei ya ofa ya sh. 15,000 badala ya sh 20,000/.

Pata kitabu hiki ili uanze kujenga nguzo hizi kisha uwe na mafanikio makubwa na ya kudumu.
Wasiliana nami: 0752 206 899.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *