Una Machaguo Mawili, Fanya Uchaguzi Bora!
Katika kuisi maisha yako una machaguo mawili, huna budi uchague moja. Uchaguzi wako leo ndiyo huamua nini ukipate kesho.
Chaguo la kwanza ni kuchukua hatua sahihi zenye maumivu kisha upate unachokitaka na kustahili.
Chaguo la pili ni kuyakwepa maumivu ya kufanya kitu sahihi sasa, lakini kuja kukutana na maumivu ya majuto baadaye. Maumivu ya majuto ni baada ya kukusa kile ulichostahili.
Kama sasa unajuta kwa kutokuwa na kitu ambacho unaamini ulitakiwa uwe nacho basi fahamu kuwa kuna muda ulikwepa maumivu na kutofanya kilichkuwa sahihi. Kwa kukwepa maumivu hayo sasa upo kwenye majuto.
Ili uweze kupata mafanikio maishani mwako huna budi kuchukua hatua zitakazo sababisha matokeo ambayo yatakuwa ni mafanikio kwako.
Hatua za kupata matokeo hayo huwa ni ngumu na zenye maumivu. Kadri unavyotaka kupata matokeo makubwa ndivyo unavyotakiwa kuchukua hatua kubwa na hapo kukubali maumivu makali.
Maumivu makali huanzia pale unapotakiwa kuchukua wajibu wa matokeo yako kwa asilimia 100. Katika hali kama hiyo hakuna mtu mwingine yoyote wa kumuachia hivyo mzigo wote hutakiwa kuwa wako. Hapo ndipo watu hukimbia na kufikiri kuna watu wengine wanawajibika kupata matokeo. Mwisho huwa majuto.
Ufanye kwa sababu unajisikia au kwa sababu ni muhimu? Kufanya kilicho sahihi huleta maumivu muda huo. Hii ni kwa sababu kuna muda hutajisikia kufanya. Lakini ukivumilia maumivu hayo kwa kujisukuma kufanya hata pale ambapo hujisikii utapata matokeo sahihi. Sababu mojawapo ya maumivu ya majuto uliyonayo sasa ni kwa sababu umekuwa ukipanga mambo lakini unafanya pale tu unapojisikia. Ukipanga fanya bila kuruhusu sababu yoyote.
Je uendelea kuishi eneo huru ili uje upate maumivu ya matokeo yale yale? Kuna kiwango cha mafanikio ulichofikia na umekaa hapo kwa muda mrefu mpaka pamekuudhi. Lakini umekuwa unakwepa maumivu ya kutoka nje ya eneo huru kwa sababu unatakiwa ufanye tofauti na ulivyozoea. Una machagua mawili ; uendelee kukaa kwenye eneo huru na kubaki na maumivu ya matokeo yaleyale madogo au uvumilie maumivu ya kufanya kwa utofauti kisha upate matokeo mapya yanayokupa amani.
Una machaguo mawili; Moja ukimbie maumivu ya kuishi ndoto yako kwa sababu ya uhitaji wa kujitoa sana au uendelee kuishi ndoto za watu wengine huku ukiacha yako ikiota nyasi. Unachagua lipi.
Ndugu! Kila jambo unaloliamua sasa lina maumivu yake hata kama huyapati lakini baadaye yatakufikia.
Umekuwa ukiyakwepa maumivu sahihi ya kuyabeba matokeo mazuri ukifikiri umefaulu, kumbe unatengeneza maumivu makili zaidi ya majuto hapo baadaye.
Chukua hatua:
Una nafasi ya kuchagua kutengeneza maisha yenye mafanikio sasa. Lakini chaguo hili litatanguliwa na maumivu. Wewe usiyakimbie maumivu hayo ukifikiri kuna mafanikio utayapata bila maumivu. Utakuja kujuta.
Chagua kitu kimoja leo unachokipenda na ambacho upo tayari kukivumilia kukifanya licha ya maumivu yake. Itapata raha na ridhiko baadaye. Hii itakusaidia usiwe mhanga wa majuto baadaye.
Unachagua nini? Chagua leo. Anza kufanya leo.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz