Ukikitamani Kitu Fanya Hivi Ili Ukipate…..
Kuna vitu umevitamani uvipate maishani. Tena kwa sababu ya kuvitamani na na kuvifikiri kwa muda mrefu, umeviota hata usiku.
Umetamani kuwa na maisha fulani hivi ambayo watu wengine hawayaoni. Umetamani kuwa na biashara fulani lakini bado hatujaiona. Umetamani kuwa mtu fulani lakini bado hajawa mtu huyo. Umetamani…..lakini…….hujawa.
Hii ni moja ya tofauti kuu ya watu waliofanikiwa na walioshindwa. Waliofanikiwa hutamani na kisha hufanikiwa kupata walichokitamani. Bali walioshindwa hutamani na kuishia kutamani. Kumbe kuna kitu kimoja kinachoamua upate unachokitamani au la! Nacho ni KAZI .
Kama hujapata kile ulichokitamani kwa siku nyingi basi tambua kuwa kazi ilikosekana.
Umetamani, umepanga umeandika nini unataka; kilichobaki ni kazi.
Hakuna mbadala wa kazi. Ndiyo maana kuna baadhi ya mipango umekuwa ukiahirisha kuianza ukifikiri kuwa na namna nyingine unayoweza kupata unachotaka.
Kazi ni rafiki wa kweli, ukimpenda lazima akupende na kukupa unachokitaka. Mpende tu……
Leo kaa chini kisha jiulize maswali yafuatayo;
Unapenda uwe na mtu wa namna gani?
Umetamani uwe na biashara gani?
Unatamani uwe na kipato gani kinachokutosheleza?
Unataka kuwa na familia ya namna gani?
Unataka kuwa na mahusiano ya namna gani?
Kisha tamani na amini kwa kiasi chochote kille ,weka mipango ya kuvipata hivyo. Kisha nenda hatua muhimu sana, weka KAZI.
Anza Leo…..Anza Sasa….Anza na Ulichonacho.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz