Anza Leo, Anza Sasa, Anza Na Ulichonacho.
Gari hufanikiwa kuwafikisha watu wanakotaka kufika endapo tu dreva atachukua hatua ya kuanza safari kwa kuliwasha gari na kuendelea na safari.
Licha ya tamaa anayoweza kuwanayo anayetaka kumiliki nyumba, lakini tamaa hiyo itatimia pale fundi atakapochukua hatua ya kuanza kuchimba msingi ambapo mwenye nyumba huyo anaweza asielewe chochote.
Ukilichukua jiwe na kuliweka sehemu litaendelea kukaa hapo milele kama hakuna nguvu ya upepo, tetemeko au nyingine yoyote itakayolilazimisha jiwe hilo hata kutikisika.
Anza Leo, Anza Sasa, Anza Na Ulichonacho! Hii ni kauli ambayo nimekuwa nikiisisitiza sana ninapokuwa naendesha mafunzo mbalimbali kama vile kuhusu kuanzisha au kukuza biashara, nidhamu, uwekezaji nk.
Hii imekuaja baada ya kuona watu wameshindwa kupiga hatua kwa sababu ya kutokuanza. Hawajaanza kwa sababu ya kuamini bado wanahitaj muda wa maandalizi lakini muda wa kuwa tayari haujawahi kufika kwako.
Lakini pia wameshindwa kuanza kwa matumaini kuwa bado wana muda wa kuanza. Hivyo mara zote wameona kama kuna fursa ya kufanya kesho.
Hii kauli umekufikia wewe leo nikiamini kuna vitu vingi ulitamani uwe umevipata au kuvifanya lakini hayo yote hayajatimia kwa sababu hukuchukua nafasi ya kuanza.
[ ] Hujaanza kuweka akiba ukiamini kipato chako ni kidogo
[ ] Hujaanza biashara ukiamini unahitaji mtaji mkubwa zaidi
[ ] Hujaanza kuamka mapema na kuipangilia siku yako na kuiishi kwa ushindi kwa sababu muda wa kujitesa hivyo bado
[ ] Hujaanza kuandika kwa sababu unaona bado huna maarifa mengi ya kuanza kuandikia
[ ] Hujaanza kuishi ndoto yako kwa sababu unaona umri haujafika
[ ] Hujaanza kuishi kwa furaha kwa sababu unaona bado kuna vitu bado hujavipata
[ ] ………
Ningweza kuendelea na orodha hii, lakini kaa chini na iendeleze orodha hii kwa kujiuliza ni vitu gani ambavyo umekuwa ukijiambia utavifanya lakini kila siku umekuwa ukiviahirisha?
Ndugu maisha yako yatabadilika sana pale utakaposema leo tena sasa naanza na chochote nilochonacho
[ ] Anza biashara kwa mtaji huohuo mdogo ulionao. Anza sasa
[ ] Anza kuweka akiba hata kwa kipato hicho unachokipata unachokiona ni kidogo sana. Anza kwa kiasi kidogo kisha ongeza kadri kipato
kinavyoongezeka
[ ] Maarifa uliyonayo yanatosha kuanza kuandika kitabu. Anza sasa
[ ] Hakuna muda mwingine, anza sasa kuanza kuamka mapema kisha kuipangilia siku yako vizuri na kuwa na ufanisi makubwa kazini.
Umesubiri vya kutosha, umechelewa vya kutosha, umeahirisha vya kutosha. Hakuna kingine kizuri kwako zaidi ya kuanza.
Dhana hii ya kuanza Leo, sasa na ulichonacho imeelezewa kiundani zaidi kwenye kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI. Nakushauri ukipate kitabu hiki Leo, tena Sasa kwa sh 10,000/ uliyonayo ili uamshe nguvu kubwa Iliyolala ndani na kuanza kupata matokeo uliyoyakosa siku nyingi.
Usisubiri muda mwingine wasiliana nasi sasa kupitia namba 0752 206 899(Alfred Mwanyika) kukipata kitabu hiki sasa.
ANZA LEO, ANZA SASA ANZA NA ULICHONACHO .
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz