Usijifariji na Udogo Wa Jicho La Jipu…Ndani Yake Ni Kubwa Sana


Categories :

Kama utatumia udogo wa jicho la jipu kuamu umakini kiasi gani uwekwe katika kushugulikia matibabu yake basi niseme utakuwa ‘umechemka’ sana.

Mlango(jicho) wa jipu huonekana ni mdogo sana ukilinganisha na ukubwa wa jipu lenyewe ndani yake. Hivyo mtu angetumia tu kigezo cha ukubwa wa mlango huo angepuuzia sana matibabu yake na kuleta madhara makubwa. Malango wake huonekana mdogo lakini jipu lenyewe huwa kubwa sana ndani.

Uuibwa wa jicho hilo huja kudhihirika pale tabibu atakapoanza kulikamua na kutoa usaa mwingi sana ndani yake na kuambatana na maumivu makali.

Matokeo ya uzembe au makosa unayoyafanya sasa ni kama mlango wa jipu yanaonekana kama ni madogo sana lakini madhara yake kwenye maisha kiujumla ni makubwa sana. Kwa mfano;

[ ] Kutowajibika kwa maisha yako huonekana kama siyo kitu kikubwa sana na kuwa maisha yanaweza kwenda. Lakini kiukweli madhara yake yamekuwa makubwa sana kwa kufanya watu kuishi maisha ya kawaida kwa kipindi chote cha uhai wao.

[ ] Kutukuweka akiba huonekana ni kitu ambacho si muhimu sana. Hii hudhihirika pale mtu anapoamua kutumia kipato chote anachopata. Lakini kuna madhara makubwa sana ya kuendelea kuishi kwenye utumwa wa fedha.

[ ] Kuchelewa kuamuka asubuhi huonekana sio tatizo na mara nyingine kuonakana kama ndiyo fahari. Lakini hiki ndicho kilichosababisha watu kuwa na siku zisizo na uzalishaji na hivyo kushindwa kupiga hatua.

[ ] Kutokusema nakupenda au asante kwa mtu wako wa karibu huonekana kama ni kitu kidogo lakini baadaye ndiyo sababu kuu ya migogoro kwenye mahusiano

[ ] Kuahirisha mambo huonekana si shida.

Lakini hicho tu ni mlango wa jipu la kukosa matokeo na kubaki hali hiyo hiyo kwa muda mrefu.
Kuanzia sasa usikidharua kitu chochote kwa kujisemea hakina madhara makubwa. Madhara ya jambo hilo ni makubwa unapoliacha kuwa sehemu ya maisha yako.

Kama kuna kitu sahihi, anza kukiisha sasa hata kama ni kidogo. Kama kuna kitu unatakiwa ukiache, acha sasa hata kama unakiona ni kidogo kiasi gani.

[ ] Anza kuwajabika kwa 100% kuhusu maisha yako

[ ] Anza kuweka akiba hata kwenye kipato kidogo

[ ] Anza kuwahi kuamka sasa. Utaiishi siku yako kwa ufanisi na kupata matokeo makubwa

[ ] Anza kumwambia nakupenda mtu wako wa karibu

Usidharu jambo lolote dogo. Kama baya usishwishike kulifanya lakini pia kama ni zuri lifanye kwa nidhamu ya hali ya juu.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *