Kama Hujafanya Maamuzi Basi Jibu Ni Hapana .
Ndugu chochote kilichotokea maishani mwako ni matokeo ya maamuzi yako. Kama umepata matokeo mazuri basi hongera kwa kufanya maamuzi sahihi.
Kuna wakati umetakiwa ufanye maamuzi kwa kusema ndiyo au hapana, lakini hukufanya hivyo. Lakini hata wakati huo ulifanya maamuzi. Na maamuzi yako yalikuwa hapana.
Maamuzi ni kitu kigumu ndiyo maana wengi huwa hawapendi kufanya maamuzi au hata wakifanya wanafanya maamuzi mabovu. Ili kuepukana na hayo umekuwa ukijinyamazisha lakini hongera kwa sababu hata muda huo ulifanya maamuzi, na yalikuwa ya hapana hata kama hukutamuka.
[ ] Pale ulipoambiwa kuwa ili uweze kuweka uelekeo sahihi wa nguvu, muda na rasilimali zako na kisha wewe hukuchukua hatua hiyo, hapo ulisema HAPANA kwenye kuweka malengo
[ ] Pale ulipoambiwa kama unataka kupata matokeo ya mafanikio maishani mwako hakikisha unajenga urafiki na kazi. Kwa sababu bado huweki kazi kwenye mipango yako, tambua kuwa umesema HAPANA kwenye kazi.
[ ] Uliambiwa kuwa ili uupate utajiri basi hakikisha unaweka akiba kwenye kila kipato. Wewe unajiona hukufanya maamuzi yoyote. Lakini kwa sababu unatumia hela yote bila kuweka akiba, basi tambua kuwa ulisema HAPANA kwenye kuweka akiba
[ ] Uneambiwa kuwa ili uweze kujihakikishia mafanikio unahitaji kuchukua uwajibikaji wa 100% . Kwa sababu umekuwa ukidhani na kuwaachia watu wengine maisha yako basi umesema HAPANA kwenye maisha yako.
[ ] Umeambiwa furaha ya kweli inatoka ndani yako na sio ya kutegemea matukio. Kwa sababu umesubiri watu au matukio yaseme ndiyo kwenye furaha tambua umechagua kusema HAPANA kwenye furaha yako ya kweli.
Hatima ya maisha yako yapo mikononi mwako. Maamuzi yako ndiyo yataamua uwe na maisha ya namna gani maishani mwako. Kuna maamuzi ya kusema ndiyoa kisha kuweka kazi.
Sema NDIYO kwenye maamuzi hayo, kutosema ndiyo kisha kuchukua hatua ni kuchagua kusema HAPANA kwenye mambo ya msingi ya maisha yako.
Sema NDIYO kwenye;
[ ] Kuwa na maono na kuweka malengo
[ ] Kuchukua uwajibikaji wa maisha yako kwa 100%
[ ] Kuwa na urafiki na kazi
[ ] Kuweka akiba
[ ] Kuwa kiongizi wa furaja yako
Je umekuwa ukisema hapana kwenye mambo gani ya msingi?
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz