Umekalia Nini?


Categories :

Kuna ombaomba mmoja aliyejulikana kukuaa eneo fulani kwa muda mrefu huku akiwaomba watu wamsaidie. Katika eneo hilo alitumia boksi ambalo lilikuwa limefungwa na mfuniko kukalia.

Licha ya kukalia boksi hilo kwa miaka mingi lakini hakuwahi kulifungua boksi hilo. Siku moja alikuja mtu mmoja msamalia akitaka kumpa fedha. Ombaomba huyo alimchangamkia akitarajia kupata kitu kutoka kwa mtu huyo.

Wakati akimsogelea ombaomba huyo, aliona kuna kitu kinang’aa sana ndani ya boksi hilo kupitia tundu dogo lililotokea baada ya boksi hilo kutumika kwa muda mrefu.

Baada ya kuuona mnga’ao huo ikabidi amauulize yule ombaomba kuwa je kilichokuwa ndani ni nini na kama ameshawahi kulifungua boksi hilo?Ombaomba yule akamjibu kuwa hajawahi kulifungua boksi hilo kwani yeye aliona linafaa kwa kukalia tu.

Ndipo yule mtu akamsihi ombaomba afungue lile boksi. Alipofanikiwa kufungua mfuniko wa lile boksi ndipo yule ombaomba alipigwa na butwaa kuona kulikuwa na dhahabu ndani yake. Alijiuliza imekuwaje amekaa na dhahabu yenye thamani kubwa kiasi kile kwa muda mrefu hivyo bila kujua?

Mtu yule akamuambia umeteseka kwa miaka mingi ukiomba fedha hata za kujikimu tu. Lakini umekuwa ukikalia kitu chenye thamani kubwa sana cha kukufanya maisha unayostahili.

Ndugu mkasa huu una fundisho kubwa sana kwako.
[ ] Umeishi maisha ya kinyonge sana kiuchumi bila kujua una utajiri mkubwa karibu yako tena ndani yako
[ ] Umewapa thamani kubwa sana watu wengine kisha wewe kujidharau angali wewe una upekee mkubwa sana ndani yako.
[ ] Umejiona huwezi kufanya chochote angali ndani yako kuna nguvu ya kutenda mambo makubwa ambayo ni miujiza kwako na kwa watu wengine
[ ] Umeomba na kutia huruma kwa watu ukiona kama wao wamependelewa, ukweli na wewe kuna kitu ambacho watu wanatakiwa wakifuate kwako.
Ndugu una hazina ya kipekee ndani yako, nayo ni UWEZO. Hii ni nguvu iliyolala tu ndani yako ikisubiri uaiamshe.

Chagua kitu kimoja au vichache unavyopenda kuvifanya, viwekee malengo kuvipata, jifunze na weka nidhamu kubwa ya kuvipata. Vumilia mpaka uvipate. Hakika vitakuwa vyako.

Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo utakaokusaidia kutambua nguvu yako ya kipekee na kisha kuiamsha na kukuwezesha kupiga hatua kubwa ambazo hujawahi kufitia. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kupata kitabu hiki.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *