Usiache Kufanya Hili Hata Mara Moja , Isije Ikageuka Kuwa Tabia Yako.


Categories :

Ndugu yangu,
Wanasema mafanikio ni tabia. Kama kuna tabia za kufanikiwa basi kuna tabia za kushindwa pia.

Ili uweze kujenga tabia yoyote unahitaji wa wastani wa siku 66. Baadhi ya tabia na watu huenda mpaka zaidi ya siku 200.

Tabia za mafanikio ni kama;
[ ] Kuchukua wajibu maisha yako
[ ] Kukweka malengo na mipango
[ ] Kuwa rafiki wa kazi
[ ] Kutokuahirisha mambo
[ ] Kujiendeleza binafsi
[ ] Kutoa thamani kwa watu wengine
[ ] Kuweka akiba
[ ] Kuwekeza
[ ] Kuwa na shukrani
[ ] Kuamka mapema

Tabia za mafanikio ni ngumu kuzijenga ukilinganisha na tabia za kushindwa. Hii ni sababu ya kwa nini watu wengi wameishia kujenga tabia za kushindwa.

Kuna mambo ya muhimu ya kufanya katika maisha yako. Haya ndiyo ya kuhakikisha unayafanya bila kuacha ili kuweza kujihakikishia mafanikio.

Inawezekana kuna tabia za mafaniko ambazo unaziishi na zimeanza kukupatia mafanikio. Ili uweze kuendelea kukuza kile ambacho umeshaanza kukivuna, kamwe usiache kuendelea kuziishi.

Kuanza kuacha kuziishi utatengeneza tabia ya kutoziishi tabia hizo za mafanikio. Kutokuziishi tabia za mafanikio ni kuchagua kuishi tabia za kushindwa.

Njia rahisi ya kukabiliana na hili ni kutokuruhusu kuacha kuishi tabia za mafanikio hata mara moja. Ukiruhusu mara ya kwanza kuna nafasi ya kuruhusu tena mara ya pili. Hivyo usijaribu kuanza kutokuishi kwani utaifanya kuwa tabia.

[ ] Usiache hata mara moja kuwahi kuamka, usije ukajenga kuwa tabia
[ ] Usiache hata mara moja kutokuweka akiba kutoka kwenye kila kipato
Hivyo kila ukitaka kuacha kuiishi tabia ya mafanikio jisukume kutokuiishi. Jiambie ngoja niiishi isije ikawa nia tabia.

Katika kukuwezesha kujenga nidhamu ya kuziishi tabia za mafanikio kila siku AMSHA UWEZO CONSULTANTS ina programu ya JENGA NIDHAMU KALI ambapo ili kuwa kwenye kundi hili unachagua tabia moja ambayo utaiishi kila siku bila kuiacha.

Ili kutithibitishia kuwa unaiishi, utaweka ushahidi kwenye kundi kila siku. Programu hii ni bureee kabisa, kazi ni kwako. Cha msingi ni kutokuiacha tabia hiyo kwa siku tatu mfululizo. Kujiunga na kundi hili haikisha una app ya telegram kwenye simu yako kisha bonyeza kiunganishi hiki; https://t.me/+uftysBbpBl4zODE0

Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *