Je Hicho Ndicho Unachokihitaji Zaidi Maishani Mwako?


Categories :

Uliposikia maneno haya ‘’unachokihitaji zaidi maishani mwako’’ kuna kitu kilikuja kwenye fikra zako kuwa hiki ndicho ninachokihitaji.

Watu wengi wana vitu fulani ndani yao ambavyo wangetamani kuvipata au kuvikamilisha kabla hawajaondoka katika dunia hii.
·       Wapo ambao wangependa waishi maisha fulani ambayo wanahisi wangefikia kilele cha furaha maishani mwao.
·       Wapi ambao wanatamani wangekuwa viongozi fulani wakubwa katika zawadi hii ya uhai waliyo nayo
·       Wapo ambao wangetamani wamiliki mali au fedha kiasi fulani na kuupata uhuru kamili kwenye maisha yao
·       Wapo ambao wangetamani watembelee maeneo fualani maarufu kabla hawajaondoka maishani mwaowapo ambao wangetamani wawasaidie kuwavusha watu wengine katika maisha yao na hivyo wangejiona ni wa thamani kubwa katika dunia hii.

Lakini nasikitika kusema asilimia kubwa ya watu wengu hawapati vile wanavyovitamani maishani mwao. Wanakufa wakiwa hawajatimiza ndoto hizo. Wapo wengine wanaofanikiwa hata kuweka malengo kabisa ya kuvipata au kufanya vitu hivyo lakini hawavifanyi.

Sababu kubwa ya kwa nini hawapati vile wanavyovitamani ni kuwa, tunavyovifanya ni tofauti na vile tunavyotakiwa kuvifanya. Tunavyotakiwa kuvifanya ndiyo hivyo ambavyo vingetupatia vile tunavyovitaka zaidi.

Abraham Lincoln alisema “Discipline is choosing between what you want now and what you want most” ikiwa na tafsiri kuwa nidhamu ni kuchagua kati ya kile unachokitaka sasa na kile unachokihitaji zaidi. Hii ndiyo sababu ya kwanini watu hawapati vile wanavyovitaka maishani mwao; wanachagua kufanya wanavyovitaka sasa.

Una ndoto kubwa ya kufika mabali, sawa hongera sana, lakini kila ulipopanga kufanya kile kitakachokusaidia kupata unachokitaka zaidi, kuna chaguo jingine linalokuvutia zaidi nalo ni kupata kile unachokitaka sasa.
Unachokitaka sasa hutamanisha sana lakini havidumu.

Unachokihitaji zaidi huhitaji muda mrefu na kazi kubwa. Ni kwa sababu hii unachokihitaji sasa kimakuwa kikwazo kikuu cha kutopata unachokihitaji zaidi.
·       Kusema NDIYO kumfurahisha mtu ni hitaji la sasa unahitaji zaidi HAPANA
·       Kutumia fedha zote kwa ANASA ni hitaji la sasa unahitaji zaidi AKIBA
·       Kuendelea KULALA sana asubuhi ni hitaji la sasa unahitaji ziadi KUAMKA MAPEMA
·       Kuendelea KUAHIRISHA kuanzisha biashara ili kujiandaa ni hitaji la sasa unahitaji zaidi KUANZA
·       Kumtafuta nani wa KUMLAUMU wa kushindwa kwako ni hitaji la sasa unahitaji zaidi KUWAJIBIKA

Ndugu kitu unachohitaji zaidi ni chenye thamani kubwa katika maisha yako, hicho ndicho kitakachokusaidia kuacha alama kubwa katika maisha yako. Kuanzia sasa anza kujiuliza kwenye kila unachotaka kufanya, je hiki ndicho ninachohitaji zaidi au nakihitaji sasa tu? Muda wote chagua kile unachohiaji zaidi.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu (Uwezo wako halisi & Mafanikio)
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *