Anza Na Hizi ANZA Kumi (10) Ushuhudie Mabadiliko Makubwa Maishani Mwako.


Categories :

Kuna laana kubwa ambayo imewakumba watu wengi. Hii ndiyo ilyowakwamisha watu wengi. Inawezekana umebaki ulipo bila ya kufika ulipotakiwa kufika kwa sababu ya laana hiyo.

Laana hiyo ni kuto KAUANZA. Kuna matokeo unayoyataka, hujayapata au umepata kiasi kidogo kuliko kwa sababu ya kuto kuanza. Kuanza kuna ukinzani mkubwa kuliko hatua nyingine.

Njia pekee ya kuondokana na laana hii ni kujisukuma kuchukua hatua ya kuanza. Unapofanikiwa kuanza unapta matokeo yale uliyotakiwa uyapate. Vifuatavyo ni vitu unavyoweza kuanza kuvifanya na vikaleta mageuzi makubwa sana maishani mwako;

1. Anza kuishi maisha yako. Unaweza ukawa unajiuliza kuwa ni kwa namna gani unaweza ukawa huishi maisha yako? Kuamua kufanya chochote kile ni kutokuishi maisha yako. Kuiga anachokifanya mwingine ni kutoishi maisha yako. Anza kuishi maisha yako kwa kufanya kile ambacho wewe unafanya kwa utofauti mkubwa ukilinganisha na watu wengine. Huko ndiko kwenye mafaniko yako makuu.

2. Anza kuweka malengo. Je huna maono unataka kufika wapia maishani mwako?Je unafanya chochote kinachokuja mbele yako? Je unaanza mwaka bila kuwa na orodha ya vitu unavyotaka kuvikamilisha? Je unaamka asubuhi na kufanya chochote kinachokuwa mbele yako? ANZA kuweka na kuyaishi malengo.

3. Anza kuweka kazi. Hata kama utaanza kuweka malengo, bila kazi ni bure. Ili kuanza kupata matokeo, ni lazima uanze na uendelee kuweka kazi. Anza kuwa rafiki mwaminifu wa kazi. Chochote unachokipanga kufanya, jisukume kukitekeleza.

4. Anza kuamka mapema. Kufanikiwa kuamka mapema ni kutangaza ushindi wa siku. Kabla dunia haijaamka na kuanza kukupa kelele nyingi, wewe amka, kumbuka na andika malengo ya maisha yako, fanya mazoezi, pangilia siku yako kisha ianze kwa ushindi. Hakika utakuwa na siku nzuri sana yenye uzalishaji mkubwa.

5. Anza kujifanyia tathmini. Huwezi kujua kama unapotea kama hujifanyii tathmini ya nini ulikipanga kufanya na umetekeleza kwa kiasi gani. Pia kujua ni changamoto gani zinakukwamisha na kwa namna gani uzikabili. Kabla hujalala jifanyie tathmini ya siku. Anza kujifanyia tathmini.

6. Anza biashara. Njia pekee ya kujenga kipato cha uhakika na cha kutosheleza ni kuwa na biashara. Kuanzisha biashara imekuwa changamoto kubwa kwa watu wengi. Tafuta tatizo linalowakabili watu na angalia namna ya kulitatua. Anzia hapo kupata wazo la biashara. Anza hata kwa mtaja mdogo.

7. Anza kuwekeza. Kwenye kila kipato unachokipata, jilipe kiasi fulani na kiwekeze. Fedha hiyo unaweza kuweka eneo ambalo litaendelea kukuzalishia na pia thamani ya fedha yako ikaongezeka. Wekeza kwenye hisa, hati fungani, biashara, ardhi nk. Anza hata kwa kiasi kidogo.

8. Anza kuweka akiba. Usitumie fedha yote unayoipata. Tenga kiasi fualani kama akiba. Kuna dharura zinaweza kujitokeza muda usiodhani. Utavuka salama kama utakuwa na akiba. Anza kuweka akiba hata 5% ya kipato chako.

9. Anza kutabasamu. Tabasamu hulipii kulitoa lakini lina thamani kubwa mno. Tabasamu ni afya yako. Tabasamu huvutia watu. Tabasamu hukufanya kupata wateja wa biashara yako. Hakikisha mtu anayeonana na wewe hakosi tabasamu lako. Anza kutabasamu leo na utaona matokeo makubwa sana.

10.Anza Leo. Umekuwa ukitafuta muda maalumu wa kuanza jambo. Ni siku nyingi zimepita. Nakushauri uanze leo, uanze sasa na uanze na ulicho nacho.

Jipatie kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI leo. Kina maarifa mazuri kuhusu nguvu ya kuanza. Si hivyo tu bali kinakuonyesha nguvu kubwa ambayo ipo ndani yako unayoweza kuanza kuiamsha leo na kukuwezesha kupata matokeo makubwa zaidi. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kupata kitabu hiki kwa bei ya ofa.

Usifikiri sana namna ya kupata kitabu hiki, anza sasa kwa kunipigia simu 0752 206 899 au bonyeza hapa https://wa.me/message/Q6IVWM4M5LFTG1 bonyeza sasa.

Asante,

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *