Je Ungependa Kupata Matokeo Yenye Kishindo? Basi Muulize Tembo Huyu…..
Mbwa na na tembo walikubaliana wabebe mimba kwa wakati mmoja ili waweze kuendeleza vizazi vyao.
Baada ya miezi mitatu tu mbwa alizaa watoto 6. Alikaa miezi mitatu akashika mimba tena na kuzaa watoto wengine 12 baada ya miezi 9 akazaa watoto wengine 12 baada ya miezi 12 akawa na mimba nyingine.
Akiwa na mimba huku akijisubiria kuzaa dazani nyingine ya watoto ndipo akaamua kumtembelea rafiki yake tembo. Alipomuuliza ni watoto wangapi ameshazaa mpaka muda huo, tembo akamjibu kuwa bado hajazaa na anaendelea kule ile mimba ya kwanza.
Mbwa akamshangaa sana na kumuuliza imekuwaje mwaka mzima ameshindwa kuzaa hata mtoto mmoja ingali yeye ana dazani za watoto na anatarajia kuongeza wengine si muda mrefu?
Tembo akamuambia kuwa wewe mbwa unahitaji muda usiozidi miezi mitatu kuzaa hata dazani ya watoto. Lakini mimi tembo nahitaji katribani miaka miwili kupata mtoto mmoja tu.
Lakini alimuambia kuwa licha ya kuzaa dazani ya watoto lakini ardhi haijatikisika na dunia haifahamu kuwa una dazani ya watoto.
Tembo aliendelea kumuambi mbwa kuwa mimi nalea mimba hii kwa muda mrefu lakini siku nitakapozaa ardhi itatetemeka kwa mtoto mkubwa atakayetoka.
Lakini hata wakati wa kukatiza barabara kila mtu na gari lilio karibu litamuona mtoto huyo. Watu watamsogelea na kumshangaa kwa ukubwa alionao. Pia magari yatasimama na kutoa heshima.
Hakuishia hapo,tembo pia akaendelea kumuambia kuwa licha ya kuwa na dazani ya watoto dunia haijashituka. Hata ulipokuwa unazaa hakuna kishindo chochote kilichojitokeza.
- Ulichokibeba ndani yako ni kikubwa sana, unaweza kuchukua muda kupata matokeo, lakini hakikisha unaendelea kukimwagilia.
- Usijilinganishe na mtu mwingine, ukiiga utazaa usichostahili
- Mara nyingi njia za haraka na mkato huleta matokeo ya kawaida ambayo hayashitui mtu yoyote
Tunasubiri kishindo cha matokeo yako.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz