Usitafute Mbadala Wa Mambo Haya Kumi(10) Isipokuwa…..


Categories :

  1. Usitafute mbadala wa upekee isipokuwa ishi WEWE HALISI. Kuna watu wamefanya vitu vikubwa na vya kipekee. Haya hawajapendelewa. Hata wewe unaweza kufanya vitu vya kipekee kabisa dunia ikakushangaa. Usiige bali tafuta vitu unavyoweza kufanya kwa utofauti mkubwa na kwa urahisi . Vifanye hivyo kwa nidhamu kali.
  2. Usitafute mbadala wa kuwajibika isipokuwa chukua jukumu la maisha yako kwa 100%.

Hakuna mtu mwingine wa kutengeneza maisha uanayoyataka isipokuwa wewe mwenyewe. Hata huyo unayedhania, ana kazi kubwa ya kujitengeneza kuwa yeye. Unataka kuwa nani? Anza kuweka kazi ya kuwa huyo unayemtaka.

  1. Usitafute mbadala wa kazi isipokuwa weka kazi.

Unataka matokeo lakini unaichukuia na kuikimbia kazi. Hapo unajidanganya. Weka mipango kisha wewe kazi, tena kazi mkubwa. Tumia akili, ndiyo, lakini baada ya hapo lazima uweke kazi. Hakuna mbadala wa kazi isipokuwa kazi yenyewe.

  1. Usitafute mbadala wa uzoefu ispokuwa kufanya.

Huwezi kubobea kwenye kile unachokifanya kwa kufanya mara moja. Huwezi kuwa na uzoefu kwa kuepuka kufanya na kukosea. Weka nidhamu ya kufanya kitu hicho mara moja aua mara chache.

  1. Usitafute mbadala wa kukuza biashara isipokuwa kukuza mauzo.

Moyo wa biashara ni mauzo. Uhai wa biashara ni mauzo. Ili kukuza biashara yako huna budi kukuza mauzo. Wafikie wateja tarajiwa wengi zaidi, wafanye wateja wako wa sasa wanunue zaidi.

  1. Usitafute mbadala wa kuweka akiba isipokuwa weka tu.

Utajiri huja kwa kutotumia kiasi chote cha kipato. Bali kwa kuhakikisha unabakisha asilimia fulani ya kila kipato unachokipata. Anza kwa kuweka hata 5% ya kipato chako.

  1. Usitafute mbadala wa kuanza, bali anza.
    Wengi wameshindwa kuanza baada ya kuendelea kutafuta muda mzuri wa kuanza. Kila wakitaka kuanza wameona kama bado hawajawa tayari. Siku, wiki, miezi na miaka sasa imepita, bado tu wanajianda. Muda mzuri wa kuanza ni leo, tena sasa kwa kutumia kile ulichonacho.
  2. Usitafuta mabadiliko bali anza kubadili mtazamo.
    Mabadiliko ndiyo huleta matokeo tofuati. Matokeo tofauti ndiyo heleta mafanikio.
    Kila mtu anashauku ya kupata mafanikio, na ili ayapate unatakiwa kufanya mabadiliko. Mabadiliko halisi ya nje yanaanza kwa kubadili mtazamo. Amini inawezekana.
  3. Usitafute mbadala wa fedha isipokuwa thamani.
    Hakuna siri tena, unataka fedha basi tafuta thamani ambayo utaitoa ili watu wengine wawe tayari kulipia. Ukitaka kuwa tajiri basi ongeza kiwango cha thamani.
  4. Ustafute mbadala wa hofu isipokuwa kufanya kile unachokihofia. Licha ya kuwa na athari kubwa , lakini hofu huyeyuka pale unapoamua kufanya kile unachokihofia.

Anza leo anza sasa na anza na ulichonacho kutotafuta mbadala wa haya mambo 10 isipokuwa kuchukua hatua unayostahili.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *