Je Unataka Kufanikiwa? Basi Ingia Kwenye Kundi(3%) La Watu Hawa.


Categories :

Ukilinganisha idadi ya watu wanataka kufanikiwa na wale waliofanikiwa ni mbingu na nchi. Licha ya tamaa ya watu kutaka kufanikiwa ni wachache sana wanaofanikiwa.

Kutotakana na utafiti ulifanyika chuo kikuuu cha Havard kuhusu malengo na mafanikio, ilionekana kuwa kuna kundi dogo la 3% lilikuwa la kipekee.

Katika utafiti huo 84% ya watu walioingia kwenye utafiti huo walikuwa hawana malengo kabisa, 13% walikuwa wana malengo lakini hawajayaandika wakati 3% pekee wakiwa na malengo yaliyoandikwa.

Hili kundi la 3% lilikuwa la kipekee kwa sababu walionekana kufanikiwa mara tatu zaidi ya wale waliokuwa na malengo yaliyokuwa hayajaandikwa.

Kumbe sababu mojawapo ya wewe kutofanikiwa inachangiwa na kutokuwa na malengo. Inawezekana una malengo lakini hayajaandikwa popote.

Steve Maraboli alisema “If you have a goal, write it down. If you do not write it down, you do not have a goal – you have a wish” ikiwa na tafsiri ya kiswahili kuwa kama una lengo basi liandike, usipoliandika basi huna lengo bali una tamanio. Hapa unaona umuhimu wa kuwa na lengo na pia kuliandika.

Kuweka malengo kunakupa dira ya wapi uelekee. Una uhaba wa muda, nguvu, umakini, fedha nk hivyo ili hivi viweze kutumika vizuri basi vipe muongozo kwa kuwa na malengo.

Kuwa na malengo ya muda mrefu kama miaka mitano, kumi, ishirini, hamsini na kuendelea. Lakini pia kuwa na melengo ya muda mfupi kama mwaka miezi sita, mitatu, mmoja.

Lakini ni muhimu sana kupata malengo ya muda mfupi zaidi kama wiki mpaka siku ili uweze kuwa na ufanisi mkubwa zaidi.

Unahitaji kuweka malengo bora ili yaweze kukupa mafanikio. Malengo bora yana sifa zifuatazo zinazojumuishwa kwenye kwa neno SMART(Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Time).

Kuna vitu unatamani uvipate katika uhai wa maisha yako, vitawezekana kama ilivyowezekana kwa watu hao wa 3%. Unachotakiwa kuanza kufanya sasa ni;

  1. Andika kitu kimoja kikubwa unachokihitaji maishani mwako(Hii ni ndoto yako)
  2. Kiwekee malengo kutoka na muda. Unataka uwe umepiga hatua gani ya lengo kuu baada ya mwaka mmoja, mitano, kumi, ishirini nk?
  3. Endelea kugawa malengo yako mpaka kwenye hatua unazoweza kuzifanya kila siku
  4. Yaandike malengo yako mara kwa mara.
  5. Yatathmini na kuboresha hatua zako kila siku.

Ndugu! Jukumu la kupata kile unachotaka ni la kwako kwa 100%. Maarifa uliyoyasoma hapa ni sehemu ndogo ya maarifa mengi na mazuri yaliyopo kwenye kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI.

Kitabu hiki kinaeleza kiundani namna ya kuweka malengo makubwa yatakayoweza kuamsha uwezo wako mkuu na kupata unachokitaka.

Si hivyo tu bali kinakupa mbinu za kuhakikisha unashugulika na malengo yako na kuyatimiza. Kitabu hiki kinapatikana kwa nakala ngumu lakini na sauti. Kipate leo ili uingie kwenye 3% ya wale walifanikiwa. Wasiliana: 0752 206 899. Au bonyeza hapa: https://wa.me/message/Q6IVWM4M5LFTG1

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *