Fumba Macho Yako Ukione Hiki……Utashangaa Sana!


Categories :

Je umewahi kujiuliza kwa nini watu hufumba macho wanapoomba?

Je umewahi kujiuliza kwa nini watu hulia huku wakiwa wamefumba macho?

Na kwa nini pia watu hucheka kwa furaha kubwa wakiwa wamefumba macho?

Kama haitoshi kwa nini mtu huota ndoto akiwa usingizini akiwa amefumba macho?

Kuna siri kubwa kwenye kufumba mambo. Unapofumba mambo unayafanya mambo yako yasitazame wala kuona vitu vinavyoonekana kwa macho ya nje bali uvione vinavyoonekana kwa macho yako ya ndani.

Sasa kama mtu hulazimika kufumba macho kwanza ili aone vya ndani, basi tambua kuwa vile vinavyoonekana kwa mambo haya ya nje vinaweza kuwa kikwazo vya vya vitu vya thamani kubwa ndani yako.

Kumbuka chochote unachoweza kukifanya huanzia ndani yaani kwenye fikra na moyo wako.

Kumbuka pia ili uweze kukua vitu ambavyo vipo nje havitakiwi vikuzuie kutazama na kuona vitu vikubwa ndani yako.

Kumbe kama hupigi hatua, kuna uwezekano mkubwa kuwa vitu vya nje yako vinakuzuia usivione vikubwa ndani yako.

Baada ya kupata mafanikio yako ya sasa, umejiona umeshafika, umeacha kuweka jitihada, vimezuia kuuona ukubwa wako ndani yako.

Mtazamo wako wa sasa wa kuona uhaba, ubaya, mapungufu kwa watu, umasikini, unyonge mbele watu unaziba usione ukuu na ujasiri ndani yako.

Kelele za nje kupitia mitandao ya kijamii zinakuzuia wewe usione wala kusikia ukuu wako wa ndani.

Hapa unahitaji kufumba macho yako ili uweze kuona wewe halisi wa ndani mwako huna budi kufumba macho yako.

  1. Kuna mafanikio umeyapata, lakini fumba macho yako jiulize kama kungekuwa hakuna kikwazo chochote je kiasi gani cha mafanikio unakihitaji, weka mipango ya kukipata hicho.
  2. Fumba macho yako fikiri kuhusu samaki baharni na hewa angani, hivi havijawahi kuisha licha ya binadamu kuvitumia kila siku. Kuna utele, na wewe unaweza kuwa tajiri.
  3. Fumba macho yako, mafaniko uliyoyapata ni kwa sababu ya kiasi ambacho akili yako imekupimia. Usijipunje jipendelee sasa. Chukua hatua;

Tafuta eneo tulivu kisha fumba macho yako na kusahau kabisa hali uliyonayo sasa. Tengeneza picha kamili ya maisha yako unayotaka uyapate bila kujali mazingira uliyonayo. Kisha weka mipango ya kuanza kuyaishi hata kwa kuchukua hatua ndogo ndogo huku ukitunza maono yako.

Anza Leo, Anza Sasa, Anza Na Ulichonacho.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *