Ziishi Siri Hizi Tano(5) za Matajiri Ili Na Wewe Uanze Kuuvuta Utajiri Wako……
Kama kuna kitu ambacho wengi wanatamani kitokee maishani mwao basi ni utajiri tena utajiri wa fedha na mali.
Lakini kama kuna kitu ambacho watu wengi wanakikosa licha ya kukitamani sana basi ni utajiri.
Watu wachache tu kati ya wengi wanaoutamani utajiri ndiyo wanaofanikiwa kuupata utajiri huo.
Hapa kutakuwa na siri kubwa kwa hawa wachache wanaofanikiwa ambazo unaweza kujifunza na wewe ukakaribisha utajiri kwenye maisha yako.
Mambo mengine wanayoyafanya matajiri hawa inaweza kuwa umeshayaona lakini kwa sababu hujayafanyia kazi, bado yanabakia kuwa siri kwako mpaka uyafanyie kazi na kukupa matokeo katika maisha yako.
Jifunze hizi siri tano(5) ambazo matajiri wanaziishi kisha zifanyie kazi katika maisha yako ili uanze kukaribisha utajiri maishani mwako.
1. Hawaahirishi mambo. Utajiri ni matokeo ya thamani unayoitoa kwa watu wengine kupitia biashara au kazi nyingine unayoifanya.
Matajiri wanatambua kuwa kuahirisha mambo ni hasara kubwa kwani unaweza kukosa matokeo kwa kuahirisha kuchukua hatua za mpango uliofanyia kazi hata kwa miaka mingi.
Ili upate matokeo na kisha kuweka nguvu, uzingativu na muda kwenye mipango mingine, usiahirishe ulichopanga kufanya.
2. Hawatangazi mipango yao kwa kila mtu. Kutaka kuwa tajiri ni mpango ambao watu wengi wameshindwa, hivyo watu wengi hawatapenda kuona wewe unafanikiwa.
Ili mipango yako ya utajiri iweze kufanikiwa hakikisha unawashirikisha watu wachache sana na ambao una uhakika wa watakuunga mkono na siyo kukuvunja moyo.
3. Wanajenga biashara na uwekezaji ambao utawapa fedha hata kama wamelala. Safari ya utajiri ni ndefu na inayokuhitaji kutoa thamani kubwa kwa wengine.
Ili uweze kufikia hatua hiyo, hakikisha unajenga biashara yenye mfumo imara ambao itaendelea kuongiza fedha hata bila uwepo wako na hata pale wewe utakapokuwa umelala.
Kwa upande mwingine fedha unazozipata bila kujali udogo wake anza kuziwekeza kwenye maeneo ambayo yatazalisha faida bila kujihusisha moja kwa moja. Maeneo kama haya ni kwenye hisa, hati fungani, biashara zenye mfumo nk
4. Hawatumia fedha zao kuwaonyesha watu wengine . Matajiri hutumia fedha zao kuzalisha fedha nyingine.
Wanafanya hivyo kwa kuzirudisha faida wanazozipata kwenye zao ili zizaliane kabisa au kwa kuwekeza maeneo mengine ambayo yataendelea kuzalisha.
Usitumie fedha hizo kigodo kuonyesha kuwa na wewe hupo nyuma. Usiendekeze starehe au kununua vitu visivyozalisha fedha nyingine.
5. Wanachagua sana. Matajiri hawafanyi chochote, hawaambatani na mtu yoyote au kusoma na kusikiliza chochote.
Bali wanawachagua marafiki wachache sana wanaowaunga mkono. Wanachagua kitu kimoja au vichache wanavyovibobea na kutoa thamani kubwa. Pia hawaingizi chochote akilini mwao. Wanachgua mambo maalumu ya kusoma. Wanahakikisha hawaingizi uchafu akilini mwao.
Ndugu! Zitafakari siri hizi tano ambazo matajiri wanazo kisha na wewe anza kuziishi. Hakikia utakaribisha utajiri maishani mwako.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz