Fanikiwa Kufanya Kitu Hiki Kigumu Ili Mafanikio Yaanze Kumiminika Kwako….
Kuwa na mafanikio makubwa ni tamanio la kila mtu. Lakini ni watu wachache sana waoyapata mafaniko wanayoyataka.
Kumbe kutakuwa na kikwazo kikubwa sana kinachosimama katikati ya matamanio hayo na mafanikio yenyewe.
Kwa jinsi wengi walivyoshindwa kupata mafanikio hayo, basi unaweza ukatabiri kuwa kizuizi hicho kitakuwa kikubwa sana na chenye nguvu kubwa.
Ungeweza kusema ni kuweka malengo, lakini kuna idadi kubwa ya watu wanaoweka malengo lakini hawafanikiwi.
Ungeweza kusema labda watu hawana nguvu za miili, lakini wapo watu wengi wenye miili yenye afya lakini hawana mafanikio makubwa.
Kumbe kikwazo kikubwa ni nini basi?
Kikwazo kikubwa na kigumu kinachozuia kutimia kwa tamaa za watu wengi ni fikra.
Kazi ngumu kuliko zote duniani ni kushawishi akili yako kuwa hicho unachotaka kufanya au kupata siyo kigumu. Hapo ndipo wengi hupata shida.
Mafanikio huanzia ndani kisha nje. Yaani lazima fikra zako ziamini kuwa unachotaka kukifanya si kigumu na hivyo unaweza kukifanya na kupata matokeo licha ya ugumu wake.
Kama akili yako isipokubali hilo, basi tambua hakuna mafanikio yoyote unayoweza kupata.
Hivyo hali uliyonayo sasa imesababishwa na yafuatayo;
- Akili yako imeamini ni vigumu kujituma na kupata mafanikio makubwa zaidi ya sasa.
- Akili yako imeona ni vigumu kuwa tajiri
- Akili yako imeamini ni vigumu kwa wewe kuwa huru hapa duniani
- Akili yako imeamini ni vigumu kutengeneza fedha
- Akili yako imeamini ni vigumu kuamka mapema
- Akili yako yako imeamini ni vigumu kuishi ndoto kubwa
- Akili yako imeamini kuwa ni vigumu kufanya mambo ya kipekee.
- Akili yako imeamini kuwa ni vigumu kuweka akiba kutoka kwenye kila kipato
Habari njema ni kuwa ukifanikiwa kuuondoa ugumu huo kuna nguvu kubwa sana itazaliwa ya kukusaidia kufanya mambo makubwa kisha matokeo makubwa.
Je ufanye nini kutoa ugumu huu?
Usiwe na wasiwasi juu ya hilo. AMSHAUWEZO Consultant tumekuandalia semina iliyobebwa na kichwa PIGA U-TURN 101 ZA MAISHA YAKO. Kupitia semina hii utatambua fikra zote zilizokuwa zinakupa ugumu wa kupata matokeo kisha kupiga U TURN(kugeuka) na kwenda uelekeo wa fikra za kukaribisha mafanikio.
Mpaka mwisho wa semina utakuwa umetambua mambo 101 yaliyokuwa yaliyokuwa yanakupa ugumu wa kupata matokeo kisha kuja na hatua 101 za kufanikiwa kuondoa ugumu huo.
Semina hii itafanyika kuanzia Julai 20 – 29, 2023 kwa njia ya kundi maalumu la wasap.
Ada ya semina hii ni sh 10,000/ unayolipia kupitia MPESA; 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Pata picha unapata hatua sahihi 101 za kubadili uelekeo wa maisha yako, lazima upige hatua kubwa sana.
Ili kujihakikishia nafasi hii nakushauri ujiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hiki; https://chat.whatsapp.com/Lmel6ehEr30K5a1S1BCEYu
Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na;
Mwl. Alfred Mwanyika
0752 206 899
www.amshauwezo.co.tz
Karibu sana.